Ukanamungu (pia:Uatheisti kutokaneno laKiyunani cha kale,atheos, likiwa na maana ya "bila miungu") kijumla ni msimamo wa kutokuwa naimani juu wa uwepo wamiungu, ama kukataa imani kuwa kuna miungu, yaani ni dhana kuwa hakunaMungu wala miungu. Hivyo ni kinyume cha Utheisti, imani kuwa angalau kuna Mungu mmoja.
Asili ya neno Uatheisti, limechipuka hata kabla yakarne ya 5, lilitumika kuwakilisha wale wasioamini uwepo wa miungu inayoabudiwa najamii kubwa yawatu, wale waliovunjwa mioyo na miungu, au wale wasioona sababu yoyote ya msingi ya kuamini uwepo wa miungu.
Neno lenyewe uatheisti lilianza kutumika hasa mnamokarne ya 16, baada ya kusambaa kwa fikra huru dhidi yadini.
Hoja zinazotetea uatheisti, zimegawanyika kwenye makundi mbalimbali yakiwemo ya kifalsafa, kijamii na kihistoria.
Mantiki ya kutoamini uwepo wa miungu inajumuisha, tatizo lauovu, hoja yafunuo zinazokinzana, na kukataadhana isiyoweza kupingika.
Wasioamini wanadai kuwa uatheisti ndio dhana asili ya binadamu kuliko Utheisti, kwa sababu kila mtu anazaliwa bila kuwa na imani ya Mungu au miungu; kwa maana hiyo basi, nijukumu la anayeamini uwepo wa miungu au Mungu kuthibitisha madai yake na si jukumu la atheisti kuthibitisha kuwa hakuna Mungu au miungu.
Tafiti za zamani kutoka shirika la habari la Uingereza (BBC), zilionyesha kuwa 8% ya watu woteduniani ni waatheisti, huku zile za zamani zaidi zikionyesha kuwa ni 2% pekee, na wale wasiokuwa na dini yoyote wakiunda 12% ya watu wote duniani.
Mwaka2015, tafiti zimeonyesha 61% ya watu waChina walikuwa waatheisti, huku tafiti za mwaka 2010 zikionyesha kuwa 20% ya watu waUmoja wa Ulaya hawaamini uwepo waroho ya aina yoyote wala miungu, hukuUfaransa naUswidi zikiongoza kwaidadi kubwa ya waatheisti, zikiunda 40% na 34% kila mmoja.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.