Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Ujain

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo la Ujain.
Sanamu ya Thirtankara hekaluni

Ujain auJina Dharma nidini yenye asili yaUhindi na wafuasi wake huitwa Wajain. Ilianzishwa mnamo mwaka500 KK.

Kuna waumini milioni 6 duniani na zaidi ya nusu wako Uhindi.

Wajain hukumbuka walimu 24 wa dini yao wanaoitwa "thirtankara". Thirtankar wa 24 alikuwaMahavira wakati wakarne ya 6 KK anayetajwa mara nyingi kamamwanzilishi wa dini hiyo, ingawa wenyewe husema hakuna aliyeanzisha hasa.

KamaUbuddha, hii ni dini isiyo na mafundisho kuhusuMungu aumiungu. Vilevile kama Ubuddha ilianzishwa katika mazingira yaUhindu wa kale ikikataa matabaka ya kidini jinsi ilivyo katika Uhindu.

Ujain unalengaukombozi wanafsi yabinadamu. Kwa ukombozi huu ni muhimu mtu ajifunze kujitawala kwa sababu kilatendo linafuatwa na mazao yake yanayoitwaKarma.

Nafsi katikaimani ya Kijain huzaliwa tena na tena katikamwili mpya, kumbe shabaha ni kutozaliwa tena, bali kupata ukombozi nastarehe yamilele.

Nafsi auroho haziko ndani ya watu pekee, lakini pia ndani yawanyama.

Kila tendo linalosababishamateso kwakiumbe mwingine linarudisha nafsi katika mzunguko wa kuzaliwa tena. Matendo yanayoharibu karma ya mtu ni hasa mauaji ya viumbe wenye nafsi.

Kwa hiyo Ujain hufundisha kuepukana nauhasama na kutomtenda yeyote kwa mabavu. Kwa sababu hiyo Wajain hukataa kulanyama, kwa kuwa nyama inapatikana kwa njia ya kuua na kutesa wanyama ambao nao ni makazi ya nafsi sawa na wanadamu.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Ujain&oldid=1337381"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp