Uhispania (Kihispania:España;Kiingereza:Spain) kwa rasmiUfalme wa Hispania, ni nchi iliyoko Kusini-magharibi mwaUlaya ikiwa na maeneo katika Kaskazini mwaAfrika. Ikiwa na sehemu ya kusini kabisa ya bara laUlaya, ni nchi kubwa zaidi katika Ulaya ya Kusini na ya nne kwa idadi ya watu miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya. Inashika maeneo makubwa yaRasi ya Iberia, na eneo lake pia linajumuisha Visiwa vyaCanary, vilivyoko Mashariki mwaBahari ya Atlantiki,Visiwa vya Balearic, vilivyoko Magharibi mwa Bahari ya Mediterranean, na miji ya kiutawala yaCeuta naMelilla, katikaAfrika.
Kunapwani ndefu yaBahari ya Mediteranea na pia yaAtlantiki.
Uhispaniabara ni sehemu kubwa yarasi ya Iberia.Visiwa vya Baleari kwenye Mediteranea naVisiwa vya Kanari katika Atlantiki pamoja namiji yaAfrika ya KaskaziniCeuta naMelilla ni sehemu za Uhispania.
Mji mkuu niMadrid ambayo ni piamji mkubwa wa nchi.
Eneo la nchi nikm² 505,990 nalo lina wakazi 47,450,795 (sensa yamwaka2020).
MfalmeFelipe VI amevaataji mwaka2014, akishika nafasi yababa yakeJuan Carlos I, anayeheshimiwa sana kwa sababu aliongozataifa katika mabadiliko ya kutokaudikteta wajeneraliFrancisco Franco kuelekeademokrasia. Hasa tendo la mfalme la kuzuiamapinduzi wa kijeshi linakumbukwa sana.
Muundo waserikali niUfalme wa Kikatiba, hivyo kisheria madaraka ya mfalme ni madogo.
Utawala umo mikononi mwaserikali inayochaguliwa nabunge linaloitwa "Las Cortes likichaguliwa kwakura za kidemokrasia.
Wakazi wa kwanza waliojulikana kwa jina kuwa waliishi Uhispania walikuwaWakelti.