Ufunuo ndio tukio au mchakato ambaomawasiliano kati yaMungu nabinadamu yanafanyika. Ufunuo ni pia yaliyomo katikaujumbe unaotokana na Mungu.
Ni kwamba katikadini mbalimbali kunaimani ya kwamba Mungu anaweza kujifunua kwa binadamu na kuwafunulia matakwa yake kwao.
Pengine ufunuo huo unakuja kuandikwa katikakitabu kitakatifu, kama vileBiblia kwaWayahudi naWakristo, naTorati,Zaburi,Injili naKurani kwaWaislamu.
Ufunuo una umuhimu mdogo katika dini nyingine, isipokuwa katikaUbuddha.
Mpokeaji
Nabii ndiye jina la mtu anayepokea ufunuo huo ili kuwajulisha wengine.
Namna za kutolewa
Namna za ufunuo kufanyika zinaweza kuwa mbalimbali, kama vile:
Kutokana naasili yake isiyo yakimaumbile, ufunuo hauwezi kuchunguzwa na mbinu zasayansi. Hata hivyo ni muhimu kupambanua ufunuo wa kweli na ule bandia ambao mtu anaweza kudanganyika au kudanganya.
Mada
Ufunuo unaweza kuhusu:
- matukio yajayo (k.mf. mwisho wadunia);
- mambo ya mbinguni kuhusu Mungu,malaika n.k.;
- ufafanuzi wa matukio ya wakati uleule.
Uyahudi
Kadiri ya dini ya Kiyahudi, Mungu alijifunua mara nyingi katikahistoria yataifa lao kamaHistoria ya Wokovu, kuanziamababu wao, lakini hasa kumpitiaMusa, asili yaTorati (vitabu vitano vya kwanza vyaBiblia ya Kiebrania).
Baada yake walitokeamanabii wengi waliokubalika kuwa wa kweli na ambao vitabu vyao vilipokewa na wengi kama vitakatifu.
Tanakh ilikamilika kwa vitabu vingine vilivyoongezwa kabla yaYesu Kristo.
Wayahudi wanaendelea kumsubiriMasiya atakayekamilisha ufunuo wao.
Ukristo
Wakristo wanapokea ufunuo wa Mungu kwa taifa laIsraeli, wakiona ujio waYesu kuwa ndiokilele chake, ambapo Mungu alijifunua si kwa njia ya manabii, bali kwa njia yaMwana wake, aliyeNeno wa milele. Katika yeye ufunuo umekamilika usiweze kuboreshwa tena. Ufunuo huo unajitokeza hasa katikaAgano Jipya.
Kwaimani hiyo, Mungu aliwahi kujifunua kwawazazi wetu wa kwanza,Adamu naEva, akaendelea hasa kwataifa laIsraeli, hadi alipomtumaMwanae ajifanye mtu wa taifa hilo teule. “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi, mwisho wa siku hizi amesema na sisi katika Mwana” (Eb 1:1-2).
Baada ya hapo, ufunuo wa Mungu hauendelei, kwa sababu alikwisha kuukamilisha kwa kumtuma dunianiNeno wake wamilele. “Kwa kuwa torati ilitolewa kwa mkono wa Musa; neema na kweli zilikuja kwa mkono wa Yesu Kristo. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote; Mungu Mwana pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyemfunua” (Yoh 1:17-18). Baada yake hauwezekani ufunuo mpya. Hatutakiwi kumuamini yeyote akidai eti, ametumwa kukamilisha kazi ya Yesu; kwa kuwa mwenyewe alisema, “Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe” (Math 24:35). “Ijapokuwa sisi au malaika wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri, na alaaniwe! Kama tulivyotangulia kusema, na sasa nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe!” (Gal 1:8-9).
Msimamo wa Kanisa Katoliki
Ufunuo huo wa Mungu unatufikia kupitiaKanisa lake, lililokabidhiwaMapokeo ya Mitume na linaloongozwa naRoho Mtakatifu hadiukweli wote. Yesu aliahidi kwamba, “Yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake” (Yoh 16:13). “Maana Roho huchunguza yote hata mafumbo ya Mungu” (1Kor 2:10).
Hivyo tupokee ufunuo wa Mungu kwa kusadiki mafundisho ya Kanisa lake, ili tuzidi kumjua na kuambatana naye bila kudanganyika. Yesu aliwaambiaMitume wake, “Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma” (Lk 10:16). “Sisi nasi twamsukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kwelikweli, litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini” (1Thes 2:13).
Tukipata mafundisho ya Kanisa tunapaswa kuyasadiki kwa moyo mmoja tupate uzima wa milele, kwa kuwa Yesu aliwaambia Mitume, “Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa” (Mk 16:16).
Tunapaswa kusadiki hasaUtatu wa Mungu pekee, kwamba ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu.Milele yote Baba kwa jinsi alivyo ndani mwake anamzaa Mwana na kumvuviaRoho Mtakatifu, kama vilejua linavyotoamwanga najoto lisitenganike navyo. Mwana, ambaye “ni mng’ao wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake” (Eb 1:3), alisema: “Nimekuja kutupa moto duniani” (Lk 12:49). Naye Roho aliwashukia wafuasi wake “kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa Roho Mtakatifu” (Mdo 2:3-4).
Katikateolojia yaKikristoneno ufunuo lina maana ya jumla yadogma zote, yaani kweli zilizofunuliwa na zinazodai imani ya kila mtu ili kupatawokovu.
KwaKanisa Katoliki kweli hizo zinapatikana katikaBiblia pamoja naMapokeo yaMitume vinavyofafanuliwa naUalimu wa kanisa.
Kanisa Katoliki linatofautisha pia huoufunuo wa hadhara namafunuo ya binafsi ambayo si lazima watu wengine wayasadiki.
Uislamu
Uislamu pia unakubali ufunuo wa Mungu kwa Wayahudi kupitia manabii, Isa (Yesu) akiwa mmojawao, lakini unaamini ufunuo huo umekamilishwa kupitiaMuhammad, nabii wa mwisho na mkuu kuliko wote, na umeandikwa katikaKurani, inayohesabiwa "neno la Mungu" kwa maana kamili, kwa kuwa limetoka kwake na kuandikwa bila mabadiliko.
 | Makala hii kuhusu mambo ya dini bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |