Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire ya Kaskazini United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland |
|---|
|
Kaulimbiu:Dieu et mon droit (Kifaransa: "Mungu na haki yangu") |
| Wimbo wa taifa:God Save the King |
Ufalme wa Muungano katika dunia Ufalme wa Muungano na Umoja wa ulaya |
Mji mkuu na mkubwa | London |
|---|
| Lugha ya taifa | Kiingereza |
|---|
| Kabila (2021) | |
|---|
| Serikali | Ufalme wa kikatiba wa bunge la umoja |
|---|
• Mfalme wa Ufalme wa Muungano | Charles III |
|---|
• Waziri Mkuu wa Ufalme wa Muungano | Keir Starmer |
|---|
Historia |
• Muungano wa Kiingereza na Kiskoti | 1 Mei 1707 |
|---|
• Muungano wa Britania na Eire | 1 Januari 1801 |
|---|
• Uanzishwaji wa Ufalme wa Muungano wa sasa | 12 Aprili 1927 |
|---|
| Eneo |
|
|---|
| • Jumla | km2 243,610(ya 80) |
|---|
| • Maji (asilimia) | 1.34% |
|---|
| Idadi ya watu |
|
|---|
| • Kadirio la 2019 | 67,545,757 |
|---|
| • Msongamano | 270.7/km2 |
|---|
| PLT (PPP) | Kadirio la 2024 |
|---|
| • Jumla | ▲ $4.28 Trilioni |
|---|
| • Kwa kila mtu | ▲ $62,570 |
|---|
| PLT (Kawaida) | Kadirio la 2024 |
|---|
| • Jumla | ▲ $3.59 Trilioni(ya 10) |
|---|
| • Kwa kila mtu | ▲ $52,420 |
|---|
| HDI (2022) | ▲ 0.940 juu sana (ya 15) |
|---|
| Sarafu | Pauni ya Sterling |
|---|
| Majira ya saa | UTC+0 Greenwich Mean Time (GMT)
|
|---|
| Upande wa magari | Kushoto |
|---|
| Msimbo wa simu | +44 |
|---|
| Jina la kikoa | .uk |
|---|
Ufalme wa Muungano wa Britania na Eire Kaskazini,Inayojulikana kwa kawaida kamaUfalme wa Muungano (UK) auBritania, ni nchi iliyoko Kaskazini Magharibi mwaUlaya, nje ya pwani ya bara kuu. InajumuishaUingereza,Uskoti,Welisi, naEire Kaskazini.Ufalme wa Muungano inajumuisha kisiwa chaBritania Kuu, sehemu ya kaskazini-mashariki ya kisiwa cha Eire, na sehemu kubwa ya visiwa vidogo ndani ya visiwa vya Britania, ikichukua eneo la maili za mraba 94,354 (kilomita za mraba 244,376).Mnamo mwaka 2023, Ufalme wa Muungano ulikadiriwa kuwa na idadi ya watu milioni 68.2.London ndio mji mkuu na jiji kubwa zaidi laUingereza na Ufalme wa Muungano.
Katikakarne zilizopita nchi iliongozamapinduzi ya viwandaduniani, ilienea katika mabara yote kwa makoloni yake mengi ikabaki hadi leo kati ya nchi muhimu zaidi ulimwenguni.Ni mwanachamamwanzilishi waUmoja wa Mataifa, ambapo anakiti cha kudumu nakura ya turufu katikaHalmashauri ya Usalama.
Miaka1974-2020 ilikuwa pia ni mwanachama waUmoja wa Ulaya; ilijiondoa baada yakura ya wananchi.
Historia
Eneo hilo lilikaliwa na watu tangu miaka 30,000 iliyopita.
Miaka 2000 iliyopita kisiwa chaBritania kilikaliwa namakabila ya Wakelti kikavamiwa naDola la Roma kuanzia mwaka43BK.Waroma wakatawala sehemu zote za kisiwa kikubwa isipokuwa Uskoti kwa miaka 400.
Walipoondoka wanajeshi wao, walowezi wapyaWagermanik kutokaUjerumani wa Kaskazini naDenmark walihamia kisiwani, wanaojulikana kamaWasaksoni naWaangli.Utamaduni wa Wakelti uliendelea katika Welisi na Uskoti.
Ndicho chanzo cha Ufalme wa Uingereza uliounganisha sehemu zilizokaliwa nawalowezi Wagermanik.
Mwaka1066Wanormani kutokaUfaransa walivamia Uingereza wakafaulu kuchukua utawala wa kusini mwa Uingereza. Uvamizi wao ulibadilisha utamaduni na pia lugha ya nchi. Walifaulu kuvamia Welisi na Uingereza lakini walishindwa kuteka Uskoti. Katika karne za utawala wao lugha ya Kiingereza ilizaliwa ambayo kimsingi bado ni lugha ya Kigermanik ya Wasaksoni pamoja na athira kubwa ya msamiati wa Kilatini-Kifaransa uliotokana na mabwana Wanormani walioshika utawala.
Tangumwaka1284Welisi ilitawaliwa na Uingereza na katika Hati ya Muungano(Act of Union) ya mwaka1536 ilikuwa rasmi sehemu ya Milki ya Uingereza.
Kutokana na asili yao katikaUfaransa ya kaskazini wafalme wa Uingereza walijaribu pia kutetea madai yao ya utawala juu ya sehemu za Ufaransa. Baada ya Vita ya Miaka 100 walipaswa kuachana na madai haya.
Katika karne ya 16 mfalme Henry VIII aliamua kutanganishaKanisa Katoliki la nchi yake kutokamamlaka ya Papa hivyo akweka misingi kwa kutokea kwaKanisa Anglikana.
Wakati huohuo mfalme wa Uingereza alipanusha utawala wake juu ya kisiwa cha Eire.
Tangu 1603 mfalme wa Uingereza alikuwa pia mfalme wa Uskoti na hati ya Muungano ya mwaka1707 iliunganisha milkimbili za Uingereza naUskoti kuwaMilki ya Britania Kuu. Tangu wakati uleule Ufalme waEire (Ireland) ilitawaliwa na Uingereza pia.
Katikati ya karne ya 17 kulikuwa navita ya wenyewe kwa wenyewe ya 1642 hadi 1648. 1649 mfalme Charles I alihukumiwa na kukatwa kichwa na kwenye Mei wa mwaka uleule Uingereza ulitangaziwa kuwa "Commonwealth" yaanijamhuri chini yaOliver Cromwell. Baada ya kifo chake ufalme ulirudishwa lakini wafalme hawakupata tena utawala kamili walipaswa kukubali kipaumbile wabunge la raia wa ufalme. Hivyo Uingereza ilikuwa mfano wa mfumo wa utawala wa sheria inayoundwa na wawakilishi wa wanachi wenyewe.
Tangu karne ya 18 Uingereza ilikuwa nchi ya kwanza iliyoona maendeleo ya teknolojia iliyoletamapinduzi ya viwandani. Utajiri wa uwezo wake ulipanuka na kuweka msingi wake wa kutawala nchi nyingi nje yake kwa mfumo wa ukoloni.
Sheria ya mwaka1800 iliunganisha Ufalme wa Britania Kuu na Ufalme wa Eire na hivyo kuunda Ufalme wa Muungano (United Kingdom of Great Britan and Ireland).
Baada yaVita vya uhuru vya Eirebunge laLondon kwa sheria ya mwaka1920 (Government of Ireland Act 1920) liligawa Ireland katika sehemu mbili za Northern Ireland na Southern Ireland.
Wabunge waliochaguliwa katika Ireland ya Kusini walijitangaza kuwa bunge la Eire na kwa mapatano ya mwaka1922uhuru wa Eire ulitambuliwa. Nchi mpya ilijiita tangu1937 "Jamhuri ya Eire" na kuendelea kama nchi ya pekee. Mikoa ya Northern Ireland iliendelea kuwa sehemu za Ufalme wa Muungano.
Mwaka1999 Uskoti, Welisi na Ireland ya Kaskazini zilirudishiwa mabunge yao ya pekee.
Uskoti ulikuwa naharakati pana ya kuondoka katika Ufalme wa Muungano lakini katikakura ya watu wa Uskoti ya mwaka2014asilimia 55 waliamua kubaki.
Kumbe kura ya wananchi wa Ufalme mzima ya mwaka2016 iliamua kuondoka katikaUmoja wa Ulaya kwa asilimia 51.9. Utekelezaji ulihitaji muda mrefu na kutimizwa tarehe31 Januari 2020.