Bendera ya Ufalme wa MerinaNembo ya Ufalme wa Merina
Ufalme wa Merina ni mlolongo wa watu ambao waliwahi kuwa watawala waBukini (sasa inafahamika zaidi kamaMadagaska) katika kipindi cha miaka themanini kuanzia mwaka1787 hadi mwaka1897.
Watawala hao wa kifalme waliweza kutekeleza mambo mbalimbali kuendeleza Bukini katika vipindi vyao kabla ya kuja kwautawala wa kigeni waUingereza naUfaransa ambao kwa kiasi fulani ulidhoofishamamlaka ya kifalme.
Bukini yakarne ya 19 ilikuwa na jumla ya makabila 18. Kabila laWamerina ndilo lililokuwa kubwa na muhimu kuliko yote. Kabila hilo lilikuwa na makazi yake katikauwanda wa juu wa kati.
Idadi ya watu katika kundi hilo ilikuwa ni moja ya sita tu ya watu wote waBukini, lakini ndio lililotawalakisiwa cha Bukini kabla ya kuchukuliwa naWafaransa.
Makabila yote yaKimalagasi (wenyeji wa Bukini) yalizungumzalugha moja na yalikuwa namila nadesturi zinazofanana, hivyo yaliweza kujengaumoja wakiutamaduni uliowafanya wawejamii moja kimsingi.
Wamerina waliwekamakao makuu ya utawala wao mjiniAntananarivo; kutoka hapo waliweza kueneza mamlaka yao katika sehemu nyingine za kisiwa hicho.
Mwaka1875, Andrianampoinimerina alijipa madaraka ya kuwa mfalme wa mojawapo ya falme zilizokuwa zikipiganavita katikaImerina ya kati baada ya kumpindua mtawala aliyepita. Kwa kutumiambinu zakidiplomasia na za kijeshi aliendelea kuzichukua tawala za jirani katikahimaya yake.
Mnamo mwaka1792 aliuhamishia mji mkuu wake hukoAntananarivo, ambapo alianza kujenga mifumo ya kisiasa na ya kijamaa ya ufalme mpya.
Baada ya mwaka1800 alianzishasera ya kuyapiga vitamajimbo mengine visiwani humo kwania ya kuyaunganisha makabila yote 18. Katika kutimizajukumu hilo, alikabiliana naupinzani wa hali ya juu kutoka kwa makabila mengine kisiwani humo kama vileWasakalava,Wabezanozano naWaambongo.
Hata hivyo, wakati wakifo chake hapo1810,Andrianampoinimerina alikuwa ameifanya tayariImerina kuwa pengine ufalme wenye nguvu zaidi kuliko falme zote katika kisiwa cha Bukini.
MfalmeRadama alirithikiti cha ufalme mwaka1810 akiwa naumri wamiaka 18. Jukumu lake la kwanza kabisa baada ya kushika ufalme lilikuwa kuyapiga makundi ya ndani ya ufalme huo yaliyoasi.
Hata hivyo, mafanikio yake makubwa zaidi yalihusiana na upanuaji wa mipaka. Alitafutanjia moja kwa moja hadibaharini ili kufanikishabiashara baina yake naWazungu na kuupanuautawala wa Merina.
Jeshi lake si tu kuwa lilitumika kuyapigamajimbo mengine, bali pia kudumishasheria nautulivu katika maeneo yaliyotekwa.
Pamoja na hayo yote, hadi mwaka1823Radama aliweza kuupanua utawala waMerina katika sehemu kubwa sana ya kisiwa hicho. Ingawa utawala wake katika kisiwa hicho chote haukukamilika, hakukuwa na kipingamizi chochote kikubwa dhidi ya kujitangaza kwake kuwa mfalme waBukini.
MalkiaRanavalona I alikuwabinamu namke wa kwanza waRadama I. Kwa kuwa alisaidiwa kupataumalkia na makabila na wakuu wa majeshi ambaoRadama aliwaondoa madarakani katikaharakati zake za kukijenga kisiwa hicho upya, washauri wake walikuwa watu waliozipingasera muhimu za mfalme aliyefariki.
Malkia Ranavalona aliendelea na upanuzi ambao Radama I aliuanzisha na kuuimarisha utawala wake katikamajimbo aliyoyateka. Kabila laWasakalava liliendelea kuupinga utawala wake.
Hatimaye majeshi yaserikali yalipowashinda machifu waSakalava, walikimbia na watu wao na kwenda kwenye visiwa vya jirani ambapo walijiweka kwenyehifadhi yaWafaransa. Hali hiyo baadaye ilikuwa ndiyomsingi wa madai yaWafaransa kwamajimbo yaliyoko magharibi mwa Bukini.
Utawala wake unaweza kuelezwa katika namna mbili. Kwa upande mmoja, ulikuwa niutawala wenye vitisho kwawamisionari na watu wengine waliotekwa na kuwa chini ya utawala wa Kimerina. Kwa upande mwingine, ulikuwa kipindi chamaendeleo makubwa yaviwanda, na ambacho kiliimarishaelimu ya Kizungu na kuiweka nchi katika mwelekeo wausasa.
Shughuli za mfalmeRadama II zilielekezwa katika kuzibadilisha sera zote zilizokuwa zinapinga mambo yaliyoletwa naWazungu ambazo mfalme aliyetangulia alikuwa akizitumia. Mwelekeo huo ulisababisha upinzani mkubwa dhidi ya utawala wake kutoka kwa watu mashuhuri nchini humo, hali iliyosababisha kuanguka kwake.
Sera ya mfalme ya kusainimikataba ya siri bila ya maofisa wake kufahamu iliongeza mashaka zaidi kwa viongozi hao. Zaidi ya hayo, kuongezeka kwa athari zawamisionari naWazungu wenginekitalani kwa mfalme hakukusaidia kitu.
Jambo lililommaliza kabisa ni jaribio lake la kuwaondoa baadhi yamaafisa waandamizi wanchi ambao ndio walikuwauti wa mgongo waserikali yake na badala yao kuwawekamarafiki wake waujanani. Hili lilifufua mlolongo mrefu wa malalamiko dhidi ya mfalme, na tarehe12 Mei1863 akauawa.
MalkiaRasoherina alitawala kuanzia mwaka1863 mpaka1868 na kufuatiwa na MalkiaRanavalona II (1868-1883). Watu hao hawakupinga uendelezaji wanchi wala hawakuwachukiaWazungu.Sera yao ya nje ililengauhuru wa nchi yao kwaimani kwamba uendelezaji wa nchi kulingana na wakati usifanywe kwa namna itakayouamila za Kimalagasi. Hivyo, serikali mpya iliazimia kufanya marekebisho muhimu katikasera za Rahama.
Pamoja na yote hayo, kisiwa hicho hatimaye kiligeuzwa kuwakoloni. Hii ni kwa kuwa, ingawasera ya kuisasisha yaBukini kwa namna fulani iliimarisha uwezo wanchi hiyo wa kuteteauhuru wake, lakini kwa ujumla sera hiyo ilidhoofishaufalme huo kwa kuongezautegemezi wake kwamataifa ya kigeni.
Rebecca L. Green:Merina. The Rosen Publishing Group, New York, 1997,ISBN 0-823-91991-9 (The heritage library of African peoples).Google Books
Matthew E. Hules, et al (2005). The Dual Origin of the Malagasy in Island Southeast Asia and East Africa: Evidence from Maternal and Paternal Lineages.American Journal of Human Genetics, 76:894-901, 2005.
Mervyn Brown (2000).A History of Madagascar. Princeton: Markus Wiener Publishers.ISBN 1-55876-292-2.
Stephen Ellis and Solofo Randrianja, Madagascar – A short history, London, 2009
Brown, M. (1978) Madagascar Rediscovered: A History from Early Times to Independence (London: Damien Tunnacliff)
Campbell, G. (1981)Madagascar and slave trade, 1850-1895, JAH