Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Udeni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kwa nchi ya Ufalme, tazamaUfalme wa Udeni.
Udeni
Danmark (Kideni)
Wimbo wa taifa: "Der er et yndigt land"
"Kong Christian stod ved højen mast" (Wimbo wa kifalme)
Udeni katika UlayaUdeni katika Ulaya
Mji mkuu
na mkubwa
Copenhagen
Lugha rasmiKideni
Kabila86.11% Wadeni
13.89% Wengine
SerikaliUfalme wa Kikatiba ya Kibunge
  Mfalme
Frederik X
  Waziri Mkuu
Mette Frederiksen
  Muungano
Karne ya 8
  Katiba ya sasa
5 Juni 1849
Eneo
  Jumlakm2 43,094(ya 130)
  Maji (asilimia)1.74%
Idadi ya watu
  Kadirio la 2024 5,982,117
  Msongamano138.8/km2
PLT (PPP)Kadirio la 2024
  Jumla $496.696 bilioni
  Kwa kila mtu $83,454
PLT (Kawaida)Kadirio la 2024
  Jumla $412.293 bilioni(ya 37)
  Kwa kila mtu $69,273
HDI (2023) 0.962
juu sana
Gini (2022)27.7
SarafuKrona ya Udeni (DKK)
Majira ya saaUTC+1 (CET) / UTC+2 (CEST)
Upande wa magariKulia
Msimbo wa simu+45
Jina la kikoa.dk

Udeni ni nchi yaKaskazini mwa Ulaya iliyoko katika eneo laSkandinavia. Inapakana naUjerumani upande wa kusini, na inazungukwa naBahari ya Kaskazini naBahari ya Baltiki. Ina idadi ya watu takriban milioni 5.9 (2024), na mji wake mkuu na mkubwa zaidi niCopenhagen, ambao pia ni kitovu chauchumi, biashara, na utamaduni. Udeni inajumuisha eneo la bara laJutland pamoja na visiwa vya Zealand,Funen na visiwa vingine vidogo. Ina mamlaka ya ndani ya kujitawala yaGreenland naVisiwa vya Faroe. Inatambulika kwa ustawi wakijamii,historia tajiri, upangaji bora wa miji, na mchango wake mkubwa katika utamaduni wa Nordic.

Udeni ina mfumo waserikali wakifalme wakikatiba unaoendeshwa nabunge la aina moja linaloitwaFolketing. Mkuu wa nchi ni mfalme, lakini mamlaka ya kiutendaji iko mikononi mwa waziri mkuu na baraza la mawaziri. Ingawa ni mwanachama waUmoja wa Ulaya, Udeni imeamua kutotumia sarafu yaeuro, na badala yake hutumiaKroni ya Kideni (DKK). Nchi hii huorodheshwa miongoni mwa mataifa yenye viwango vya juu vya maisha,elimu bora, huduma za afya zenye upatikanaji mpana, na ulinzi wa mazingira.Uchumi wake una msingi imara unaotegemea sekta kama vile nishati mbadala, viwanda vya dawa, usafirishaji wa baharini, na teknolojia ya kisasa.

Jiografia

[hariri |hariri chanzo]

Udeni ina eneo lakm² 43.000.Theluthi ya eneo hili ni kwenye visiwa 443 vya Udeni ambavyo 76 tu kati yake vinakaliwa na watu.

Visiwa vikubwa niFunen (Fyn),Zealand (Sjælland) naBornholm (Bornholm).

Rasi yaJutland ni sehemu kubwa ya eneo. Jutland ni Udeni bara. Inaurefu wakm 300 kuelekea kaskazini kutokampaka wa Ujerumani hadincha yake kwaSkagen.

Kwa jumla Udeni ikotambarare. Mwinuko wa juu unakimo wam 170 pekee juu yaUB.

Kumbuka kwamba orodha hii inahusu Udeni tu kama nchi, siVisiwa vya Faroe naGreenland.[1][2]Mlima mrefu wa ufalme mzima niGunnbjørn, Greenland, m 3,700 juu yaUB.

NoMwinukoSehemu ya NchiKimo
1.MøllehøjSkanderborg manisipaa170,86 d
2.Yding SkovhøjHorsens manisipaa170,77 d
3.Ejer Bavnehøj170,35 d
4.Lindbjerg170,08 d
5.Basi Margretelyst169,78 d
6.Vistofte169,44 d

Mpaka mwaka1847Himmelbjerget,Skanderborgs, m 147 ilifikiriwa kuwa mwinuko mkubwa wa Udeni.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Wakazi wa kwanza waliojulikana katikahistoria kwa jina ni makabila yaWakimbri naWateutonia waliohamia hadi Ulaya ya kusini wakati wanjaa mnamo mwaka113 KK.

Katikakarne ya 8 hadikarne ya 11BK majambazi wa baharini kutoka Udeni na Norway waliogopwa kote Ulaya kwa jina la "Waviking". Walivamia piaUingereza mara kwa mara na kujenga makao huko. Tangu mwaka793 walitawala eneo la Danelag (au:Danelaw) kaskazini na kaskazini-mashariki mwa Uingereza wa leo.

Katikakarne ya 8 nakarne ya 10 maeneo madogo yaliunganishwa. Wafalme wa kwanza wanaojulikana kutawala Udeni yote walikuwaGarm Mzee naHarald Jino Buluu (mnamo mwaka980). Harald alikuwa mfalme wa kwanza wa kupokeaUkristo waKanisa Katoliki.

Udeni ikawa nchi yenye nguvu katika Skandinavia na kwenye pwani za Baltiki.

Kuanzia1397 hadi1521 nchi zote za Skandinavia ziliunganishwa katikamaungano ya kifalme chini ya wafalme wa Udeni ilhali kila nchi ilijitawala katika mambo ya ndani.

Baada ya Uswidi kujitenga na umoja huo, Norway iliendela kuwa chini ya Udeni hadi mwaka1814.

Mwaka1537 Udeni ilijiunga naMatengenezo ya Kiprotestanti naKanisa la Kilutheri likawadini rasmi nchini hadi leo, ikifuatwa na 76.9% za wakazi. Udeni ilikuwa kati ya nchi muhimu sana ya Ulutheri, lakini leo 3% tu wanashirikiibada yaJumapili.

Baada yavita zaNapoleoni Udeni iliondolewa utawala wa Norway iliyounganishwa na Uswidi mwaka 1814. Lakini makoloni ya Greenland, Iceland, Faroe na visiwa vyaKaribi zilibaki chini yake.

Karne ya 19 ililetafitina na Ujerumani juu ya utawala waSchleswig naHolstein. Baada ya vita ya1864 Udeni ilipaswa kuacha majimbo hayo mawili kwa Ujerumani.

Udeni haikushiriki katikaVita Kuu ya Dunia ya Kwanza lakini ilirudishwa sehemu ya kaskazini ya jimbo la Schleswig.

Wakati waVita Kuu ya Dunia ya Pili Udeni ilivamiwa na Ujerumani mwaka1940 hadi1945. Wakati wa vitaIceland iliamua kutangazauhuru wake.

Mwaka1948 mara baada ya vita visiwa vyaFaroe vilipewamadaraka ya kujitawala lakini vilibaki ndani ya umoja na Udeni. Koloni laGreenland lilipewa madaraka hayo mwaka1979.

Udeni ikawa kati ya nchi zilizoundaUM na piaNATO.

Mwaka1973 ikajiunga naJumuiya ya Ulaya (sasa:Umoja wa Ulaya), lakini imekataa kutumiaeuro badala ya krona.

Kutokana nauzazi mdogo, miaka ya mwishouhamiaji umeongezeka, hivi 12.3% wana asili ya kigeni (yaani hatamzazi wao mmoja niraia na mzaliwa wa Udeni).

Watu

[hariri |hariri chanzo]

MnamoSeptemba2024, wakazi walikuwa 5,982,117. Kati yao, Wadeni asili ni 88,67%. Wengine ni wahamiaji (kutokaUturuki,Polandi,Syria,Ujerumani,Iraq,Romania,Lebanoni,Pakistan,Bosnia na Herzegovina,Somalia n.k.) au wamezaliwa na mhamiaji walau mmoja.

Lugha ya nchi niKideni, jamii yaKijerumaniki, na 86% za wakazi huongea vizuriKiingereza kamalugha ya pili.

Upande wadini, wengi niWakristo, lakini 3% tu wanashirikiibada yaJumapili na 19% tu wanaona dini ni muhimumaishani.Dini rasmi niKanisa la Udeni (la Kilutheri; 71.2%).Wakatoliki hawafikii 1%. Kutokana nauhamiaji,Waislamu ni 4.4%.

Watu maarufu

[hariri |hariri chanzo]

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. "kort & Matrikelstyrelsen, nyt højeste punkt i Danmark". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2006-10-10. Iliwekwa mnamo2017-11-07.
  2. Faktoider.nu, Danmarks högsta punkt

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  • (Kidenmark) Busck, Steen and Poulsen, Henning (ed.), "Danmarks historie  – i grundtræk", Aarhus Universitetsforlag, 2002,ISBN 87-7288-941-1
  • (Kidenmark)Gammelgaard, Frederik; Sørensen, Niels (1998).Danmark – en demokratisk stat. Alinea.ISBN 87-23-00280-8.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help)
  • (Kidenmark)Jørgensen, Gitte (1995).Sådan styres Danmark. Flachs.ISBN 87-7826-031-0.{{cite book}}:Invalid|ref=harv (help)
  • (Kidenmark) Michaelsen, Karsten Kjer, "Politikens bog om Danmarks oldtid", Politikens Forlag (1. bogklubudgave), 2002,ISBN 87-00-69328-6
  • (Kiswidi) Nationalencyklopedin, vol. 4, Bokförlaget Bra Böcker, 2000,ISBN 91-7024-619-X.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Serikali
Ramani
Biashara
Vyombo vya habari
Mengineyo
  • Vifanord.de – library of scientific information on the Nordic and Baltic countries.


Nchi zaUmoja wa UlayaBendera ya Umoja wa Ulaya
Austria |Bulgaria |Eire |Estonia |Hispania |Hungaria |Italia |Kroatia |Kupro |Latvia |Lituanya |Luxemburg |Malta |Polandi |Slovakia |Slovenia |Romania |Ubelgiji |Ucheki |Udeni |Ufaransa |Ufini |Ugiriki |Uholanzi |Ujerumani |Ureno |Uswidi
Nchi huru
Nchi zisizokubaliwa
na umma wa kimataifa
Maeneo yanayojitawala
chini ya nchi nyingine
1 nchi yaAsia ya Magharibi kijiografia ambayo huhesabiwa kuwa sehemu yaUlaya kiutamaduni2nchi ya kimabara
Makala hii kuhusu maeneo yaUlaya bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuUdeni kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Udeni&oldid=1420577"
Jamii:
Jamii zilizofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp