Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Uchawi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mganga wa kienyeji wakabila laWashona hukoZimbabwe.
Mchoro waJohn William Waterhouse,1886 kuhusu uchawi.
Mchoro katikaMonasteri yaRila,Bulgaria, unaolaani uchawi naushirikina.

Uchawi (kwaKiingereza "Witchcraft") ninguvu zinazotumiwa na watu wenye maarifa maalumu yasiyo yakisayansi katikajamii nyingiduniani (zikiwemo zaAfrika,Asia,Ulaya n.k.), ingawa kuna tofauti nyingi kulingana na mahali au utamaduni.

Lengo lake ni kujaribubahati ya mtu na kujilinda na maadui wengine kimazingara, au kwa ajili ya kujifurahisha, japo wenyeimani potofu hulichukulia maanani na kupandikiza chuki kwa ndugu jamaa hata jirani kuwa ni mchawi.

Kwa mujibu wavitabu vyadini uwezo na nguvu zote za asili ni zaMuumba wambingu naardhi na vyote vilivyomo, hivyo yeye anampamwanadamu uwezo kadiri tofautitofauti kama apendavyo, kwa maana uwezo huo hufanyakazi katika hali ya kubahatisha, yaani ni bahati, hakuna mwenyemamlaka ya kuongoza uwezo huo wa asili ilaMwenyezi Mungu.

Kadiri ya dini mbalimbali watu wote wanaotumia nguvu hizo za asili katika hali (hasi) wapo kinyume naMunguMuumbaji wambingu nadunia, hawajui kuwa yeye ndiye mwanzilishi wa nguvu zote za asili ikiwa ni pamoja na wanadamu.

Elimu pia inaweza kusaidia kuondoa imani hizo kwani hata baadhi yamadhehebu ya dini zinachochea kuziamini imani hizo. Wasomi wakarne ya 21 wanapinga imani hizo potofu ambazo zimesababishamateso kwawazee wasio na hatia hasavijijini wakishtumiwa uchawi. Tena kumekuwa na mafarakano nachuki katika jamii nafamilia mbalimbali kwa ajili ya imani ya uchawi; kwa mfano, watu kuuana, kuharibianamali namifugo kwa kuhisiana uchawi kwa sababu ya watu waliopandikizwa imani za kishirikina.

Serikali yaTanzania imetumia jitihada zaidi pamoja na kuelimisha wananchi hasa kutokana na suala la imani potofu na tafsiri mbaya ya uchawi ambayo imepelekea watu takribani 5000 kupotezauhai toka mwaka1961 kutokana na mateso, kuchomewanyumba na vibanda katikamikoa yaTabora,Kigoma,Shinyanga na mikoa mingine; ni vilevile katika sehemu mbalimbali zaAfrika ya Mashariki naya Kati. Mwaka2008Rais wa TanzaniaJakaya Kikwete alilaani uchawi kama chanzo chamauaji ya maalbino 25. Imani hizo potofu ni maarufu hata kwa viongozi japo kwasiri.

Tazama pia

Marejeo

Marejeo mengine

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Simple English Wiktionary
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuUchawi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Uchawi&oldid=1300584"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp