Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Ubao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ubao ulioandaliwa kuwakuni
Mti huu unaonyesha miviringo 27 ya miaka yake ya kukua pamoja na safu ya nje ya ubao laini pamoja na kiini cha katikati

Ubao ni dutu inayofanya gogo na matawi yamti. Ina matumizi muhimu kwaujenzi na vifaa pia kamakuni kwamoto.

Ubao hutengenezwa na mti wakati wa kukua. Ubao laini katika ganda la nje la gogo hupitisha maji na lishe kutoka mizizi kwenda kwenye matawi na majani. Kila mwaka ganda jipya linaongezeka nje na ganda la ndani huwa imara na kupoteza uwezo wa kupitisha maji. Mabadiliko haya ya kila mwaka huonekana katika miviringo ya ubao ndani ya mti.

Ubao umetumiwa na wanadamu tangu miaka maelfu. Mwanzoni ilitumiwa kama kuni na fimbo yasilaha. Baadaye watu walijifunza kuchonga ubao kwa matumizi mbalimbali kama vileujenzi, vifaa,sanaa kamauchongaji,karatasi na mengi mengine.

Ubao huwa na faida ni imara lakini si vigumu ya kukata na kuchonga, tena ni nyepesi. Pia unapatikana kwa wingi angalau katika maeneo ambako miti inakua.

Tazama pia

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Ubao&oldid=1019028"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp