Ubaguzi wa rangi ni kitendo cha kuthamini au kutengabinadamu kwa misingi ya rangi zangozi. Ubaguzi wa rangi ulikuwa maarufu sana katika nchi kamaAfrika Kusini kwa jina la "apartheid" naMarekani kwa jina la "segregation" ambapo huko Waafrika walikandamizwa kutokana na rangi yao katika kupata huduma mbalimbali za kijamii na kimaendeleo.
Wakati wa ukoloni, rangi ilitumika kama msingi wa utoaji huduma muhimu mfano: shule, matibabu na haki nyingine za kibinadamu. Rangi nyeusi ilipewa hadhi ya chini zaidi.
Siku hizi katika karibunchi zote,sheria zinapinga ubaguzi wa rangi. Lakini katika nchi nyingi bado kuna wabaguzi wachache ambao wanavunja sheria kwa kuendelea kubagua. Kwa mfano, kuna wabaguzi wanaobaguaWatu weusi nchiniMarekani, nchini China, nchini India na katika nchi zaUlaya.
Ubaguzi dhidi ya Waafrika, haswa wale wenye asili ya Kiafrika wanaoishi nje ya bara, unashutumiwa mara kwa mara lakini haujakoma.
Makala hii kuhusu mambo yasiasa bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuUbaguzi wa rangi Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.