Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Tungamo ya Jua

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ulinganifu wa masi za nyota: nyota kibete nyekundu (M 0.1), Jua, nyota kibete buluu (M 8) na R136a (M 300)

Tungamo ya Jua (ing.Solar mass) inatajatungamo yaJua letu ambayo ni takribankilogramu 1.99 × 1030 . Hii inalingana na tungamo ya Dunia yetu mara 332,946.

Kiwango hiki hutumiwa kamakizio katika sayansi yaastronomia kwa kutaja tungamo ya magimba kwenyeanga ya nje hasanyota,fungunyota nagalaksi.

Nyota nyingi huwa na tungamo baina ya x0.1 na x10 ya tungamo ya Jua. Mara chache kuna nyota kubwa sana yenye tungamo x250 za Jua. Hivyo Jua letu liko kwenye wastani wa tungamo za nyota kati yanyota za safu kuu.

Ilhali tungamo ya Jua inaendelea kupungua polepole kutokana na mnururisho naupepo wa Jua kuna ufafanuzi waUmoja wa Kimataifa wa Astronomia wa kuhesabu tungamo ya Jua kuwakilogramu 1.9891×1030[1].

Alama yake niM ambako "M" inamaanisha "tungamo" na ☉ ni ishara ya Jua.

Vizio vinavyolingana

Tungamo moja ya Jua inalingana na

  • 27,068,510 x tungamo yaMweziM
  • 332,946 x tungamo yaDuniaM
  • 1,048 x tungamo yaMshtariiM.

Njia Nyeupe (galaksi yetu) ina takriban milioni 180 tungamo za Jua ambayo inalingana na kilogramu 3.6 · 1041.


Marejeo

  1. Measuring the Universe - The IAU and astronomical units, tovuti yaUkia, iliangaliwa Novemba 2017
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Tungamo_ya_Jua&oldid=1308738"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp