Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Tungamo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tungamo
Jiwe la kg 2 linalotumika katikamizani ili kupimiauzito.
Alama za kawaida
m{\displaystyle m}
Kizio cha SIkilogramu

Tungamo (pia:masi, kutokaKiingereza:mass) katikaelimu yafizikia nitabia yamaada, na kwa njia hii pia tabia yagimba audutu.

Kipimo sanifu cha kimataifa cha tungamo nikilogramu.Alama yake katikafomula kwa kawaida nim{\displaystyle m}.

Tungamo na uzito

[hariri |hariri chanzo]

Tungamo ni tofauti na uzito lakini katikamaisha ya kawaida hatuoni tofauti. Hivyo tunatumiakipimo cha kilogramu pia kwa kutaja uzito wasukari tunayonunua. Lakini hali halisi uzito wa gimba au Tungamo ileile ni tofauti kutegemeana na uvutano mahali ilipo. Kwa mfanomtu akifika juu yaMwezi uzito ni sehemu yasita ya uzito wakeduniani. Kwa hiyo mtu mwenye uzito wa kilogramu 60 duniani atakuwa na kilogramu 10 pekee akipimwa juu ya Mwezi. Sababu yake ni ya kwambauvutano wa Mwezi ni ndogo kuliko duniani.

Tungamo na uvutano

[hariri |hariri chanzo]

Uvutano wa gimba fulani unategemeana na tungamo yake. Kila kitu hata gimba dogo kamajiwe,meza au mtu lina uvutano wake. Ila tu tungamo kubwa yaDunia yetu inafanya uvutano wake yaani nguvu inayosababisha ya kwamba watu na vitu havieleihewani bali kukaa kwenye uso wa ardhi tukivutwa kuelekeakitovu chasayari yetu. Vitu vyote vinavyoshikwa na uvutano wa Dunia vina uvutano wao vilevile lakini kwa sababu tungamo ya watu na vitu ni ndogo kabisa kuliko tungamo ya Dunia hatuwezi kusikia tofauti. Pia Mwezi unavutwa na graviti ya Dunia yetu lakini tungamo ya Mwezi ni kubwa kiasi kwamba uvutano waMwezi unaathiri pia Dunia. Hii inaonekana kirahisi kutokana na mabadiliko yabahari kuwamaji kujaa na kupwa yanayosababishwa na uvutano wa uvutano wa Mwezi.

Tungamo na inesha

[hariri |hariri chanzo]

Tungamo inafanya piainesha ya gimba fulani. Inesha ni tabia ya tungamo kubaki katika hali yake ya kutulia au kuwa na mwendo fulani hadi iathiriwe na nguvu ya nje. Tungamo kubwa zaidi huwa na inesha kubwa zaidi na inahitaji nguvu kubwa zaidi kwa kubadilisha mwendo wake. Tunaiona kwa urahisi tukijaribu kusukumabaisikeli,gari aulori: tungamo zake ni tofauti, hivyo nguvu inayohitajika kuzisukuma au kuzisimamisha inatofautiana.

Makala hii kuhusu mambo yafizikia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuTungamo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Tungamo&oldid=1326824"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp