Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Tokyo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Tokyo
Bendera ya Tokyo
Bendera ya Tokyo
Mahali pa Tokyo katika Japani
Shibuya
Marunouchi
Idadi ya wakazi

Jiji la Tokyo (東京都) nimji mkuu waJapani. Takriban watumilioni 12 huishi katikajiji hilo ambao ni sawa 10% ya Wajapani wote.Rundiko la mji lina wakazi milioni 35 na ni rundiko kubwaduniani.

Tokyo nikitovu cha Japani upande wabiashara,uchumi nasiasa.

Mahali pa jiji nitambarare ya Kanto kando yahori ya Tokyo.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Awali Tokyo iliitwa "Edo". Wakati uleKyoto ilikuwa mji mkuu rasmi na mahali paTenno auKaisari wa Japani. Edo ilikuwa mwanzonibandari ndogo tu. Ilianza kukua baada ya kuwa makao makuu ya Mashogun waliokuwaviongozi wa kijeshi katika Japani.

Katikakarne ya 19Tenno Meiji alihamisha mji mkuu kwenda Edo iliyoitwa "Tokyo" yaani "mji mkuu wa mashariki". Mji ulikuwa na tayari mwishoni mwakarne ya 19 ulikuwa mji mkubwa wa pili duniani baada yaLondon.

Tokyo iliharibiwa namoto katikahistoria yake, pia namatetemeko ya ardhi namabomu wakati waVita Kuu ya Pili ya Dunia. Ilijengwa upya na kukua kuwa jiji kubwa duniani.

Ilikuwa mahali pamichezo yaOlimpiki ya mwaka1964.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo yaJapani bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuTokyo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Tokyo&oldid=1386794"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp