Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Theta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kigiriki
Herufi za kawaida
Α α Alfa1Ν ν Ni50
Β β Beta2Ξ ξ Ksi60
Γ γ Gamma3Ο ο Omikron70
Δ δ Delta4Π π Pai80
Ε ε Epsilon5Ρ ρ Rho100
Ζ ζ Dzeta7Σ σ ς Sigma200
Η η Eta8Τ τ Tau300
Θ θ Theta9Υ υ Ipsilon400
Ι ι Iota10Φ φ Phi500
Κ κ Kappa20Χ χ Khi600
Λλ Lambda30Ψ ψ Psi700
Μ μ Mi40Ω ω Omega800
Herufi za kihistoria1
Digamma6San90
Stigma6Koppa90
Heta8Sampi900
Yot10Sho900
1 Viungo vya nje:
Alfabeti_ya_Kigiriki#Viungo_vya_nje

Theta niherufi ya nane katikaAlfabeti ya Kigiriki. Theta kubwaΘ ina umbo la "O" yenye mstari wa katikati. Theta ndogoθ ina umbo la duaradufu nyembamba pamoja na mstari lala wa katikati lakini kuna pia umbo lisilofungwa kamaϑ.

Kwa matumizi yatarakimu inamaanisha namba 9.[1]

Matamshi yake siku hizi ni sawa na "th" kwa Kiswahili.

Matumizi ya kisayansi

[hariri |hariri chanzo]

Jinsi ilivyo kawaida na herufi mbalimbali za kigiriki inatumiwa kama kifupi kwa ajili ya dhana mbalimbali katika hesabu na sayansi. Mifano kadhaa ni

  • katika fani yafizikia
    • Theta ndogo θ au ϑ ni alama ya halijoto
    • Theta ndogo ni alama kwa kiwango chapembe katika usokotaji.
    • Theta kubwa Θ hutumiwa kama alama ya kuonyesha nguvu ya uga magnetiki
  • katika fani yaastronomia
    • Theta kubwa Θ inatajasaa za nyota
    • Theta ndogo ϑ hutaja nyota inayoonekana kwenye nafasi ya tisa katikakundinyota kulingana na nguvu ya nuru yake.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Theta ina maana ya tisa ingawa siku hizi ni herufi ya nane. Sababu yake ni ya kwamba alama yadigamma imepotea katika alfabeti lakini imebaki kama tarakimu ya sita
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Theta&oldid=933699"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp