Tarantula |
---|

Tarantula-miti (Encyocratella olivacea) |
Uainishaji wa kisayansi |
---|
|
Ngazi za chini |
---|
Nusufamilia 15: - AcanthopelminaePickard-Cambridge, 1897
- AviculariinaeSimon, 1874
- EumenophorinaePocock, 1897
- HarpactirinaePocock, 1897
- IschnocolinaeSimon, 1892
- OrnithoctoninaePocock, 1895
- PoecilotheriinaeSimon, 1892
- PsalmopoeinaeSamm &Schmidt, 2010
- SchismatothelinaeGuadanucci, 2014
- SelenocosmiinaeSimon, 1889
- SelenogyrinaeHirst, 1908
- StromatopelminaeSchmidt, 1993
- TheraphosinaeThorell, 1869
- ThrigmopoeinaePocock, 1900
|
Tarantula nispishi zabuibui katikafamiliaTheraphosidae wanusuodaOpisthothelae. Spishi zanusufamiliaHarpactirinae huitwabui-nyani. Spishi nyingi ni kubwa hadi kubwa sana na zote zinamanyoya marefu mengi. Kwa kawaida huwinda kwa kuvamiamawindo.
Ingawa spishi fulani za tarantula zinaweza kuwa ndogo kamamm 5, takriban zote ni kubwa hadi kubwa sana, Kwa kweli, spishi kadhaa zinaweza kufikiasm 11 zenye upana wamiguu wa sm 30 na uzito wag 170.Chonge zinaweza kufikia urefu wa sm 3.8.
Kama buibui wote, tarantula wana miguu 8,macho 8 na sehemu mbili zamwili,kefalothoraksi auprosoma nafumbatio auopisthosoma, zilizounganishwa napediseli. Chonge zinaelekea chini wima badala ya chonge zinazopitana za buibui wengi wengine. Pia, kinyume na wale wa mwisho, wanachuchu mbili au nne za kukalidi badala ya sita.
Tarantula wote wanasumu ambayo hutumia kupooza au kuua mawindo yao. Kwa kawaida sumu hiyo haisababishi zaidi yahisia inayowaka kwawanadamu wakati wanaumwa. Walakini, spishi nyingine zina sumu kali zaidi ambayo inaweza kusababisha usumbufu mkubwa unaodumusiku kadhaa.Dalili za kawaida nimikakamao namikazo mikali yamisuli.Bui-nyani mwekundu (Pelinobius muticus) anaweza kusababishamaruerue mabaya. Pamoja na sumu,protini nyingine huingizwa pia na hizi zinaweza kusababisha athari zamzio ambazo zinaweza kutishamaisha.Vidonda vya kuchomwa vinaweza kuambukizwa nabakteria ikiwa vidonda havitasafishwa vizuri.
Spishi zaDunia ya Kale hutukuta sana na kuwa na haraka kwa kushambulia. Zaidi ya hayo wana sumu kali sana. Kabla ya kuuma huchukua mkao wa kutishia kwa kunyanyua prosoma yao, kuinua miguu ya mbele juu na kupanua chonge zao. Spishi fulani hutoa piasauti ya kuchata kwa njia ya kufikicha manyoya magumu kwenyekelisera zao.
Spishi zaDunia Mpya hazina haraka sana kuuma. Badala ya hiyo hutumia manyoya maalum kwenye opisthosoma yao inayoitwa manyoya ya kuchomea, ambayo hutumika kama kinga dhidi yambuai. Wanaweza kuyatupa kuelekea adui kwa miguu yao au kuyasugua dhidi ya lengo. Manyoya hayo yanavizari na hutumika ili kuwasha. Mara nyingi yanauavipanya. Watu wengi ni nyeti kwa manyoya hayo na kupata kuwasha kali nambati. Kuyavuta na kuingia kwao machoni inapaswa kuepukwa kabisa. Lau kama manyoya yanaposhindwa kumzuia mbuai, tarantula hawa huamua kuuma.
Tarantula hula kila kitu wanachoweza kupataporini na kilicho kidogo kuliko wao. Kwa kawaidainvertebrata wadogo hushikwa, kamawadudu, lakinivertebrata wadogo, kama vipanya nawatambaazi, huliwa pia. Wanaweza kukamatandege wadogo lakini hii imeripotiwa mara chache tu. Kinyume na buibui wengi wengine tarantula hawafanyimitandao. Spishi kadhaa hufunika makao kwa tabaka nyembamba yahariri na spishi nyingine hunyumbuanyuzi za kukwaza ili kugundua mawindo, lakini mawindo huwa yanachupiwa kila wakati. Manyoya ya tarantula yana jukumu kubwa katika hiyo. Sio tu ukubwa na mahali pa mawindo, lakini pia umbali umedhamiriwa na machunguzi ya manyoya yenye hisia. Aghalabu hayo yapo miguuni lakini pia kwenye sehemu zakinywa.Tarantula huingiza sumu na maji yammeng'enyo ndani ya mawindo ili kumpooza na mtawalia kumyeyusha, na kisha kufyonzakioevu kilichomo. Kilichobaki cha mawindo nikitonge kinachofanana nakidonge kilichotapikwa nabundi k.m. chenye sehemu ngumu zilizovunjika. Machunguzi ya buibui kifungoni yalionyesha kuwa huweka vitonge hivi kila mara mahali pamoja.Takamwili za buibui ni kioevu na huondoka buibui kupitia ncha ya fumbatio.Tarantula-miti wanaweza kufyatua takamwili kwa lengo ikiwa watafadhaika.
Tarantula, wachanga haswa, huwa na maadui wengi, kama ndege, watambaazi na wanyama wengine ambao huishi kwa kutegema invertebrata wadogo. Violezo vipevu mara nyingi hawana maadui wengi sana, lakinimamalia fulani wakubwa mbuai kamarakuni,nyegere,vinyegere navicheche hufukua tarantula kabla ya kuwaua na kuwala.Maadui muhimu wa buibui wengi, pamoja na tarantula, ninyigu wa familiaPompilidae wanaoitwawauabuibui mara nyingi. Baada ya buibui kugunduliwa hupoozwa na kuzikwa kwenye kishimo au kufichwa katika sehemu zamimea kamamashina yenye matundu. Kisha nyigu hutagamayai yake na baadayemabuu hula buibui kutoka ndani akiwa hai. Wauabuibui wengi huwinda buibui wadogo, lakini spishi kadhaa zimetabahari katika tarantula. Mifano ni nyigu wa jenasiHemipepsis (spishi kadhaa katikaAfrika ya Mashariki).
- Anoploscelus celeripes,Tarantula wa Tanganyika
- Anoploscelus lesserti,Tarantula wa Rwanda
- Encyocratella olivacea,Tarantula-miti
- Eucratoscelus constrictus,Bui-nyani Kijivu
- Eucratoscelus pachypus,Bui-nyani Miguu-minene
- Heterothele affinis,Tarantula ???
- Heterothele spinipes,Tarantula Miguu-miiba
- Loxomphalia rubida,Tarantula wa Zanzibar
- Pelinobius muticus,Bui-nyani Mwekundu
- Pterinochilus alluaudi,Bui-nyani wa Alluaud
- Pterinochilus andrewsmithi,Bui-nyani wa Smith
- Pterinochilus chordatus,Bui-nyani Kijivukijani
- Pterinochilus lugardi,Bui-nyani wa Lugar
- Pterinochilus murinus,Bui-nyani Dhahabu
- Pterinochilus raygabrieli,Bui-nyani wa Gabriel
- Pterinochilus vorax,Bui-nyani Mkali
Bui-nyani mwekundu
Bui-nyani kijivukijani
Bui-nyani dhahabu