Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Taliban

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bendera nyeupe ya Taliban inaonyesha maneno yashahada.
Wapiganaji wa Taliban, wakati wa kukera kwa 2021.
Polisi wa kidini wa Taliban wakimpiga mwanamke kwa sababu alivua burka hadharani, mnamo mwaka 2001.
Taliban akimuua mwanamke hadharani ambaye alikuwa ameshtakiwa kumuua mumewe, 1998. Mume huyo alikuwa mkali, na alikuwa akimpiga na kumfungia kwa miaka mitatu.[1]
Maeneo yaliyotawaliwa na Taliban mnamo 1996 (kijani).

Taliban niharakati ya kidini, kisiasa na kijeshi yaWaislamu Wasunni iliyoanzishwa mnamomwaka1994 wakati wavita ya wenyewe kwa wenyewe nchiniAfghanistan.

Ilitawala sehemu kubwa ya Afghanistan kati ya miaka 1996 na 2001 na baada ya kuondolewa madarakani na uvamizi waMarekani mnamo2001 iliendesha vita dhidi yamajeshi yaNATO pamoja naserikali mpya ya nchi. Mwaka 2021 ilishinda tena na kuchukuautawala wa Afghanistan.

Harakati hiyo ina wafuasi wengi piakaskazinimagharibi mwaPakistan, hasa kati yaWapashtuni.

Chanzo

[hariri |hariri chanzo]

Harakati ya Taliban ilianzishwa naMullah Mohammed Omar mjiniKandahar kusini mwa Afghanistan pamoja nawanafunzi wamadrasa yake. Wanafunzi wa madrasa huitwa "taliban" kwalugha yaKiajemi. Shabaha yao ilikuwa kumaliza vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa kutumiasharia ya Kiislamu. Wafuasi wake walishinda vikundi vingine nchini hadi kutwaamji mkuuKabul mnamo Septemba 1996 walipotangazaEmirati ya Kiislamu ya Afghanistan. Katika vita hiyo Taliban walipata msaada wa siri kutoka Pakistan.

Utawala wa 1996-2001

[hariri |hariri chanzo]

Taliban ilitawala Afghanistan kati ya 1996 na 2001. Wakati huo, viongozi wake walianzisha utawala uliofuata mafundisho juu yajamii na aina yasharia yenyekanuni kali kuliko nchi zote za Kiislamu[2][3][4][5]. Ukosoaji mwingi wa Taliban ulitoka kwawasomi muhimu wa Kiislamu.[6]

Walitumia kanuni zahadd katikaurithi wa Kiislamu kama kukatamkono wamwizi, kuuamajambazi na kuuawazinzi kwa kuwapigamawe.Adhabu hizo zilitolewa mara kwa mara biladaawa yaani bilakesi kuendesha kwa utaratibu.

Wanaume walipaswa kuingiamsikitini wakiwa nje ya nyumba wakati wasala.

Hasa namna yao ya kuwatendeawasichana nawanawake kwa jumla ilishtusha watu wengiduniani na pia wenyeji wengi katikamiji ya nchi hiyo[7]:

  • Kuanziaumri wa miaka nane, wanawake hawakupaswa kuwasiliana na wanaume ambao si wa familia zao za moja kwa moja, au ambao hawajaolewa nao.
  • Hawakuruhusiwa kutoka kwenyenyumba wasipotembea pamoja namume aundugu wafamilia yao.
  • Hawakupaswa kuonekana hadharani, bila kuvaaburka ambayo ni aina yahijabu inayofunikamwili wote pamoja nakichwa nauso.
  • Hawakupaswa kuvaaviatu vya visigino virefu, ili wanaume wasiweze kuwasikia wakati wanatembea na kuamshahisia zakingono.
  • Hawakuruhusiwa kusema kwasauti kubwa hadharani, ili mgeni asiisikie.[8]
  • Madirisha yote kwenyeghorofa ya chini ya nyumba lazima yafungwe, ili wanawake wasionekane kwa wanaume wanapopitamtaani.
  • Kuchukuapicha za wanawake au kutengenezasinema zinazoonyesha wanawake kulikuwa marufuku. Hii inatumika pia kuhusu picha za wanawake kwenyemajarida,vitabu,magazeti au kwenyemaduka.
  • Wanawake hawakurusiwa kusishiriki mikutano ya hadhara.

Kwa jumla Taliban hawakutambuahaki za binadamu kwa wanawake[9].Shule za wasichana zilifungwa na wanawake hawakuruhusiwa kufanyakazi nje ya nyumba.

Kila aina yasanaa,muziki naburudani zilipigwa marufuku kabisa chini ya utawala wao.Sanamu,uchoraji,picha,kamera,runinga, n.k. ziliharibiwa.[10]

Kaskazini mwa nchivita iliendelea kwa sababu wananchi wa kule walipigana kwasilaha dhidi ya Taliban.

Kupinduliwa kwa Taliban 2001

[hariri |hariri chanzo]

Katika kipindi cha vita hiyo wapiganaji wenyeitikadi kali kutoka Pakistan naUarabuni walikuja kuwasaidia Taliban. Kati yao alikuwa piaOsama bin Laden aliyeundakundi laAl-Qaeda nchini Afghanistan na kupanga mashambulio yake dhidi yaMarekani. Baada yamashambulizi ya11 Septemba2001Marekani ilidai Afghanistan imtolee bin Laden kwao lakini Taliban walikataa wakidai kuona kwanzaushahidi. Hatua hiyo ilifuatwa na uvamizi wa Marekani. Lengo la uvamizi huo lilikuwa kuondoa serikali ya Taliban, kuharibu al-Qaeda na kumkamata bin Laden. Hadi mwisho wa mwaka 2001, Taliban walishindwa kote nchini na kujifichamlimani au kukimbilia Pakistan.

Kurudi kwa Taliban

[hariri |hariri chanzo]

Ilhali Marekani pamoja na nchi nyingine zaNATO zilikabidhimadaraka mengi kwa serikali mpya ya kizalendo, Taliban walianza upya kushambulia jeshi la wageni kutoka milima ya mpakani mwa Pakistan wakitumia mara nyingi mbinu zakigaidi na kusababishavifo vingi kati yaraia[11].

Tangu mwaka2010 walianza kudhibiti tena maeneo kadhaa yavijijini katika milima ya nchi.

Katika miaka iliyofuata walizidi kushambulia jeshi la serikali ya Afghanistan na majeshi ya Marekani na nchi za NATO. Nchi za kigeni zilianza kupunguzaidadi yawanajeshi wao kwatumaini kwamba serikali ya Afghanistan itaweza kujitetea.

Ushindi wa pili

[hariri |hariri chanzo]

Mnamo Februari2020, serikali ya raisDonald Trump wa Marekani na Taliban walitiasainiMkataba wa Doha ambamo Marekani ingeondoaaskari wote kutoka Afghanistan ifikapo1 Mei 2021.[12] Rais mpya wa MarekaniJoe Biden alitangaza kuwa kuondoka kwa nchi yake kutoka Afghanistan kutaanza Mei 1, 2021 na kumalizika mnamo Septemba 11, 2021, ambayo itakuwa miaka 20 haswa tangu mashambulio ya 11 Septemba.[13] Taliban waliahidi kutoshambulia wanajeshi wa Marekani lakini waliongeza mashambulio yao dhidi ya jeshi la serikali.

Baada ya kuondoka kwa wanajeshi wa NATO na idadi kubwa ya Wamarekani, Taliban walianza kuvamia maeneo mengi ilhali nguvu ya jeshi la kitaifa liliporomoka. Mnamo15 Agosti 2021, rais wa Afghanistan aliondoka nchini na Taliban waliteka Kabul.

Mwisho wa Agosti 2021, Taliban walidhibiti nchi yote isipokuwa jimbo laPanjshir, wapinzani walipojipanga chini ya aliyekuwa makamu wa raisAmrullah Saleh aliyetangaza kwamba amechukua nafasi ya rais kufuatana nakatiba ya jamhuri.[14]

Baada ya kutwaa Kabul, wasemaji wa Taliban walitangaza kwamba wanataka kufuatasiasa tofauti kiasi na ile ya zamani. Wasemaji walidai kwamba wataruhusu wanawake kufanya kazi na wasichana kusoma, kama wanakubali kuvaahijabu. Walitangaza pia kwamba watasamehe wananchi wote waliowahi kupigana nao. Hata hivyo, Waafghanistan wengi walijaribu kukimbia nchi kwa njia mbalimbali.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. "ZARMINA'S STORY".www.rawa.org. Iliwekwa mnamo2021-08-17.
  2. "Machtwechsel in Afghanistan - Das Frauenbild der Taliban".Schweizer Radio und Fernsehen (SRF) (kwa Kijerumani). 2021-08-17. Iliwekwa mnamo2021-08-17.
  3. Mohammad, Azadah Raz."As the Taliban returns, 20 years of progress for women looks set to disappear overnight".The Conversation (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo2021-08-17.
  4. Narain, Vrinda."The world must not look away as the Taliban sexually enslaves women and girls".The Conversation (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo2021-08-17.
  5. Hoodfar, Homa."Taliban 'has not changed,' say women facing subjugation in areas of Afghanistan under its extremist rule".The Conversation (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo2021-08-17.
  6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2021-08-19. Iliwekwa mnamo2021-08-19.
  7. Michael Griffin (2001).Reaping the Whirlwind: The Taliban movement in Afghanistan. London: Pluto Press, pp6-11/159-165.
  8. "some of the restrictions imposed by Taliban in Afghanistan".www.rawa.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2017-07-03. Iliwekwa mnamo2021-08-19.
  9. Dupree Hatch, Nancy. "Afghan Women under the Taliban" in Maley, William.Fundamentalism Reborn? Afghanistan and the Taliban. London: Hurst and Company, 2001, pp. 145–166.
  10. "The Death of the Buddhas of Bamiyan".Middle East Institute.
  11. https://www.fdd.org/analysis/2010/08/10/un-taliban-responsible-for-76-of-deaths-in-afghanistan/ UN: Taliban Responsible for 76% of Deaths in Afghanistan , August 10, 2010 , The Weekly Standard
  12. "Can the US exit Afghanistan?".Can the US exit Afghanistan?.
  13. CNN, Kevin Liptak."Biden announces troops will leave Afghanistan by September 11: 'It's time to end America's longest war'".CNN.{{cite web}}:|author= has generic name (help)
  14. "Afghan Vice President Saleh Declares Himself Caretaker President; Reaches Out To Leaders for Support".News18 (kwa Kiingereza). 17 Agosti 2021. Iliwekwa mnamo17 Agosti 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Taliban&oldid=1345951"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp