Uchafu wa anga karibu naDunia kwa mtazamo wa juu-chini.Wingu la katikati ni vitu vilivyo kwenye obiti ya chini ya Dunia, napete pembeni ni vitu kwenye obiti ya geostationary.
Takataka ya angani ni jumla yavitu vilivyo naasili katikakazi yabinadamu, vilivyopo kwenyeanga-nje na ambavyo havina manufaa tena.
Mifano nisatelaiti ambazo hazifanyi kazi tena, zilizovunjika, sehemu zaroketi, vipande vyametali vilivyokuja kama sehemu za roketi, na mengine mengi. Vitu hivi vyote hutazamwa kamatakataka hasa katikaobiti yaaninjia za satelaiti za kuzungukaDunia kwa sababu vipande vile vinaendelea kuzunguka Dunia kwenye obiti hizo. Takataka hiyo ni hatari kwa satelaiti,kituo cha anga na piawanaanga waliopo kwenye obiti kwa sababu migongano inatokea.
Hatari inatokana hasa nakasi kubwa ya vitu vilivyopo kwenye obiti ambayo ni takribankm 27,000 kwa saa[1]. Hii ni mara 10-20 kasi yarisasi yabunduki.
Hadi sasa mgongano wa satelaiti mbili umetokea mara moja tu, moja ilikuwa satelaiti iliyokufa tayari na nyingine ilikuwa satelaiti mpya[2]. Lakini satelaiti zimewahi kupigwa na vipande vidogo mara kadhaa.
Kituo cha Anga cha Kimataifa (ISS) kinaukuta maradufu; kompyuta duniani hukadiria njia yake pamoja na njia za vipande vikubwa vya takataka; kama vipande vikubwa vinaonekana kukaribia ISS, kituo kinashushwa au kupandishwa kidogo kwa kutumianozeli za gesi; kama hali hatarishi inaonekana wanaanga wanaweza kuhamia kwenye chomboanga cha Soyuz kilichopo muda wote kwenye ISS kwa hali ya dharura. Kama mwanaanga angepigwa na kipande kidogo cha takataka akiwa nje ya kituo, hatari ya kufa ni kubwa.
Ngazi ya juu ya roketi Delta II ya Marekani iliyopeleka satelaiti kwenye obiti, ikabaki angani.
Vyanzo vya takataka ya angani ni pamoja na:
satelaiti zilizokufa
ngazi za juu za roketi zilizopeleka satelaiti hadi obiti na kubaki humo baada ya kutengana na satelaiti yenyewe
vipande vidogo kamaskrubu nabolti vinavyoachana na roketi wakati wa kutengana na satelaiti
vipande vya satelaiti na roketi vinavyotokana namilipuko(body break up)[3]
vipande vya satelaiti vinavyotokana na majaribio ya kijeshi, kama vile kuharibu satelaiti kwa roketi kutoka duniani kama jaribio la kulenga, au kwabomu
vipande vinavyotokea baada ya kugongana kwa takataka na kuvunjika
Idadi ya vipande vya takataka ambavyo ni vikubwa kulikosentimita 1 hukadiriwa kuwa karibumilioni moja[4]; vipande vidogo zaidi ya sentimita hukadiriwa kuwa milioni nyingi.
Satelaiti ya Vanguard 1 ya 1958, itakayoendelea kuzunguka Dunia kwa miaka 200
Takataka ya angani ilianza kwa satelaiti zisizo na kazi tena. Mfano wa zamani zaidi ni satelaiti ya Vanguard I. Satelaiti hiyo ilipelekwa naMarekani kwenye anga-nje mwaka1958. Kazi yake ilikuwa kurushaishara zaredio duniani.Vifaa vyake zake vilifanya kazi hadi mwaka1964, baadaye ishara zake zilizimika. Tangu miaka 60 haina kazi tena lakini bado inazunguka Dunia, pamoja na sehemu ya roketi iliyoibeba hadi obiti yake[5].
Wakati ule, miaka 60 iliyopita, hakuna aliyeyaita mabaki hayo takataka. Hadi leo mambo yamekuwa tofauti. Leo hii kuna zaidi ya satelaiti 6,000 zinazozunguka Dunia yetu kwenye anga-nje. Zaidi yanusu ya idadi hiyo haina kazi tena.Fueli imekwisha,betri zimekufa,mitambo ndani yake imeharibika, ni mibovu lakini bado iko tu.
Vitu vyote vinavyozunguka Dunia kwenye obiti ya chini vinakutana namolekuli zahewa ambazo zinasababishamsuguano.Kiwango chake ni kidogo lakini kila chombo au pia kipande cha takataka kinachogusana na molekuli za hewa kitapungua mwendo wake kidogo. Kwa hiyo polepole kasi inapungua na chombo kinaanza kushuka chini na hatimaye, baada ya miaka kadhaa, kuingia katikaangahewa lenyewe. Hapo msuguano huwa mkubwa na kusababishajoto kali. Kama satelaiti si kubwa sana itaungua kabisa hewani kamakimondo. Kama ni kubwa vipande kadhaa vinaweza kubaki na kuangukia uso wa Dunia.
Kadriumbali wake ni mkubwa muda wa kubaki kwenye obiti unaongezeka hadikarne au zaidi.
Satelaiti kwenye obiti za mbali zinaandaliwa ya kupelekwa katika obiti ya takataka ambayo ni mbali zaidi. Hapotaasisi inayomiliki chombo cha aina hiyo itatumia fueli ya mwisho kukirusha tena kwenye obiti ya mbali itakapoendelea kwamilenia bila kuumbuka satelaiti mpya.
Kuna taasisi mbalimbali zinazotunza orodha za vitu vilivyorushwa angani.Umoja wa Mataifa[6] Ofisi ya NORAD yajeshi la Marekani ina orodha yasafari zote za kuelekea angani na vitu vilivyo kwenye obiti ya Dunia, pamoja na sehemu kubwa kiasi za taka, kama sehemu za juu za roketi.