Clifford Joseph Harris Jr. (amezaliwa tar.25 Septemba1980) ni rapa wa muziki a hip hop, mwigizaji, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa muziki na mmiliki wa studio yaGrand Hustle Records. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama T.I. pia humwita T.I.P.
T.I. ni rapaMwafrika-Mwamerika kutoka mitaa ya Westside Bankhead Zone 1Kusini mwa Marekani. Jina lake halisi la kisanii ni T.I.P., linatokana jina lake la utani wakati wa udogo wake "Tip", ambalo alipewa na babu yake.
Kuvuma kwake kwa, kulipelekea washabiki wake kulichukua jina lake "poa poa", ikamlazimu kulibadilisha na kuliita "T.I.P". Pindi alipotia saini mkataba na studio yaArista Records inayosaidiwa na studio yaLaFace Records mnamo 2001, akalifupisha jina lake na kuliita T.I. kwa heshima na taazima ya mwanamuziki mwezake aitwaye Q-Tip.
Pia anafahamika kwa mtindo wake wa kutembea na "Rababendi" na kujitangazia kuwa yeye ndiyo "Mfalme wa Kusini" (ambapo imeleta matatizo mengi ya hapa na pale na baadhi ya marapa wengine waishio kusini humo). T.I. ana watoto watano. Majina yao ni Messiah Ya'Majesty Harris, Domani Uriah Harris, Deyjah Harris, Clifford Joseph "King" Harris III, na Major Harris.