Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Sudan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
جمهورية السودان
Jumhuriyat as-Sudan

Republic of the Sudan
Bendera ya SudanNembo ya Sudan
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa: Al-Nasr Lana (Kiarabu: Ushindi ni Wetu)
Wimbo wa taifa: نحن جند للہ جند الوطنNahnu Jund Allah Jund Al-watan ("Sisi ni Jeshi ya Mungu na Nchi yetu")
Lokeshen ya Sudan
Mji mkuuKhartoum
15°00 N 30°00 E
Mji mkubwa nchiniOmdurman
Lugha rasmiKiarabu
Serikali
Abdel Fattah al-Burhan
Abdalla Hamdok
Uhuru
 - Tarehe
KutokaMisri naUingereza
1 Januari1956
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,886,068 km² (ya 16)
5%
Idadi ya watu
 -Julai 2015 kadirio
 -2008 sensa
 - Msongamano wa watu
 
40,235,000 (ya 35)
30,894,000
16.4/km² (195)
FedhaDinar (SDD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
MSK (UTC+3)
not observed (UTC+3)
Intaneti TLD.sd
Kodi ya simu+249

-


Sudan,rasmiJamhuri ya Sudan ni nchi iliyoka kati Afrika Kaskazini-Mashariki na ni ya tatu kwa ukubwa katikabara laAfrika na yakumi na sitaduniani.Imepakana naMisrikaskazini,Bahari ya Shamu kaskazini-mashariki,Eritrea naEthiopia mashariki,Sudan Kusinikusini-mashariki,Afrika ya Kati naChadimagharibi, naLibya kaskazini-magharibi.Mji mkuu niKhartoum.

Majimbo yaSudan Kusini yalikuwa sehemu ya nchi hiyo lakini yalipigakura ya kujitenga yakapata kuwanchi huru kuanzia tarehe9 Julai2011.

Aliyekuwa makamu wa RaisJohn Garang, ambaye awali aliongoza wanamgambo wa Sudan Kusini kupiganiauhuru wa majimbo ya kusini.

Jiografia

Ona pia:Orodha ya mito ya Sudan,Orodha ya miji Sudan

Mlima wa Dair eneo ya kati, Sudan
Bwawa kusini mwa Sudan

Sudan iko upande waAfrika ya kaskazini, inapwani kwenyebahari ya Shamu kati yaMisri naEritrea. Imetamalikiwa zaidi namtoNile namikono yake.

Ina eneo lakilomita mraba 1,886,068 (sq mi 728,215).

Ardhi yenyewe nikiwara, lakini kunamilima upande wa mashariki na magharibi.

Hali yaanga ni yamwangaza kusini, namikuranga kaskazini.

Mvua yapatikana miezi yaAprili naOktoba.

Uharibifu wa mazingira hasa ni kwa sababu yammomonyoko waudongo nautapakazi wajangwa.

Majimbo

Nchi imegawiwa katikawilaya 18, zilizogawiwa tena katikakata 133.

Historia

Sanamu ya Mfalme wa Wanubi, Sudan
Muhammad al-Mahdi
Dola la Mahdi 1881-1898

Historia ya awali

Nchi ilikuwa na makazi ya kudumu kuanziamilenia ya 8 KK.

Katikamilenia ya 5 KK watu walizidi kuhamaSahara ikigeukajangwa wakasogea katika eneo la Sudan ya sasa (bonde lamto Nile).

Mchanganyiko wa watu hao uliundaufalme wa Kush kwenye1700 KK.Makao makuu yalikuwaKerma.

Katikakarne ya 8 KK watu wa ufalme huo waliteka Misri na kuitawala kwakarne moja hadi waliposhindwa naWaashuru.

Baadaye makao makuu yalikuwaMeroe, ambapo ufalme uliendelea hadikarne ya 4BK ukiwa maarufu kwauhunzi kwa jina la Ethiopia.

Ufalme kusambaratika

Ufalme huo uliposambaratika, zilitokea falme mbalimbali katika eneo lake, mmojawapo ukiwa ule waNubia.

HukoUkristo ulienea katikamadhehebu tofauti:yale ya Kikopti kutoka Misri nayale ya Kibizanti kutokaRoma ya mashariki.

BaadayeUislamu pia ulijitokeza katika falme hizo ukazidi kuenea hadi kuanzishausultani wa Sennar.

Mwaka1821 mtawala wa Misri chini yahimaya yaWaturuki aliteka Sudan kaskazini.

Katikamiaka ya 1870juhudi zaWazungu za kukomeshabiashara ya utumwa zilisababisha kutokea kwaMahdi.

Dola la Mahdi

Dola la Mahdi (kwaKiarabu المهدية, "mahdiyya") lilianzishwa naMuhammad Ahmad Al-Mahdi mwaka1881 alipojitangaza kuwa mahdi kufuatana na imani ya Kiislamu akaongozauasi dhidi ya Misri iliyotawala Sudan ikisimamiwa yenyewe naUingereza.

Muhammad Ahmad Al-Mahdi alifaulu kukusanya wafuasi wengi na kushinda Wamisri. Tarehe26 Januari1885 jeshi lake lilitwaa mji mkuuKhartum na kumwua gavanaGordon Pasha.

Al-Mahdi alianzisha mji mkuu mpya ng'ambo ya mto Nile kwa kuundaOmdurman. Wamisri na Waingereza wakatoka nje ya Sudan.

Baada ya ushindi wake Al-Mahdi alikufa nahoma ya matumbo.

Ugomvi ulitokea kati ya makamu wake hadi1891 wakatiAbdallahi ibn Muhammad mwenye sifa ya kuwa aliongoza jeshi la mahdi wakati wa mashambulio dhidi ya Khartum alikubaliwa wa viongozi wa mahdiyya akajiita "khalifa".

Khalifa Abdullahi aliimarisha utawala wake wa kuwaua wapinzani bila neema, kati yao wanafunzi na ndugu za mahdi mwenyewe. Akajenga jumba mjini Omdurman linalosimama hadi leo.

Khalifa Abdullahi alijaribu kutumia teknolojia mbalimbali. Akanunua meli za mvuke za mtoni alizoziona Waingereza walizitumia pia akajenga kiwanda cha kutengenezea bunduki. Akaanzisha nyaya za mawasilaino kwa simu. Lakini kwa ujumla vita na utawala wa mahdiyya zilikuwa ziliharubu uchumi iliyoendelea kuzorota.

Khalifa alifaulu kupanua utawala wake juu ya maeneo karibu yote ya Sudan ya leo lakini alishindwa kufikiajimbo la Ikweta ambakoEmin Pasha aliendelea kutetea mabaki ya Sudani ya Kimisri.

Jeshi la Mahdiyya

Itikadi ya kupanua utawala wa mahdiyya kwa njia yajihad ilimsababisha khalifa kushambulia nchi jirani yaEthiopia iliyotawaliwa nakaisari wa Kikristo. Mwaka 1887 akaongoza jeshi la askari 60,000 hadiGondar. Waethiopia wakajibu kwa kushambulia Sudan mwaka 1889. Kifo cha KaisariYohane IV katika mapigano yaMetemma tarehe9 Machi 1889 ililazimisha Waethiopia kurudi kwao. Lakini jeshi la mahdiyya lilipoteza wanajeshi wengi pia likadhoofika.

Wakati huohuo jemadari wa khalifa Abd ar-Raħmān an-Nujumī alishambulia Misri lakini alishindwa kwenye mapigano ya Tushkah. Hii ilikuwa mara ya kwanza ya jeshi la mahdiyya kushindwa.

Majaribio ya vita za jihadi dhidi yaWabelgiji katika jimbo la Ikweta na dhidi yaWaitalia katika Eritrea yalishindikana pia.

Mapigano ya Omdurman 2 Septemba 1898

Mwaka1895 mkuu wa jeshi la pamoja la Misri na Uingereza, jeneraliHoratio Kitchener aliamua kulipizakisasi kwa vita ya 1885 akaongoza jeshi kubwa dhidi ya Sudan. Kwa kutumia meli za mvuke kwenye mto Nile na kujenga reli akasongea mbele hadi Omdurman.

Tarehe2 Septemba1898 jeshi la mahdiyya lilishindwa kabisa katika mapigano ya masaa matano. Safari hiyo Waingereza waliandaliwa vizuri zaidi, pia silaha mpya kamabunduki ya mtombo ziliwapa ushindi. Upande wa khalifa walikufaaskari 11,000, upande wa Waingereza na Wamisri watu 400 pekee.

Khalifa mwenyewe alitoroka akajenga jeshi upya na kutawala kusini mwa Sudan, lakini akauawa mwaka1899 katika mapigano yaUmm Diwaykarat.

Hivyo Waingereza walitawala Sudan pamoja na Misri hadi 1956, na Kitchener akawa gavana mkuu wa kwanza.

Baada ya Uhuru

Ramani ya siasa ya Sudan kabla ya Sudan Kusini kujitenga.

Baada yauhuru wa nchi (1956), makabila ya kusini, ambayo hayakukubali kusilimishwa, yalipiganiavita ndefu hadi kupata uhuru wao.

Darfur ni eneo lenye majimbo matatu ambayo imeathiriwa na vita vya kisiasa,vita vya Darfur.

Kutokana na vita nyingiserikali hazikuwa imara na kulikuwa na mabadiliko ya mara kwa mara baada ya uhuru.Mapinduzi ya kijeshi ya kwanza yalitokea mwaka1958, kishajeneraliIbrahim Abboud alitawala hadi1964 wakati alipopaswa kujiuzulu kutokana na upanuzi wa vita katika Sudan Kusini na upinzani wa wananchi kwenye mji mkuu.

Utawala wa Nimeiry

Kilichofuata kilikuwa kipindi cha serikali 3 za kiraia hadi1969. Tarehe25 Mei1969jeshi, chini yakanaliGaafar Nimeiry, lilipindua tena serikali. Nimeiry alikuwawaziri mkuu, wakatibunge na vyama vyote vilipigwa marufuku. Nimeiry alitawala hadi1985, na tangu1971 alikuwa rais. Mwaka1972 alifaulu kumaliza awamu ya kwanza ya vita ya wenyewe kwa wenyewe dhidi ya Sudan Kusini kwamapatano ya Addis Ababa. Sudan Kusini ilipewamamlaka ya kujitawala katika mambo ya ndani chini ya serikali ya kieneo.

Mwanzoni Nimeiry alijaribu kuigasiasa yaGamal Abdel Nasser nchini Misri na kutekeleza sera kadhaa zaujamaa.Utawala wake uliona upinzani kutoka kwaWakomunisti na pia kutokaWaislamu wenyeitikadi kali. Baada ya kupinduliwa kwa siku kadhaa na Wakomunisti alivunja ushirikiano naUrusi na kuanza kupokeawanasiasa wenye mwelekeo wa Uislamu mkali katika serikali yake.

Tangumiaka ya 1980 alisogea zaidi upande wa Uislamu wa kisiasa. Mwaka1983 alitangazasharia kuwamsingi washeria zote na kubadilisha sheria zajinai ipasavyo. Hatua hii ilisababisha upinzani katika sehemu za nchi zisizokaliwa na Waislamu. Alivunja pia serikali ya kieneo kwa Sudan Kusini na hivyo vita ya wenyewe kwa wenywewe ilianza upya.

Nimeiry alitangaza hali ya dharura iliyompa tena mamlaka zakidikteta. Mwaka1985 aliruhusu kunyongwa kwamwanafalsafa MwislamuMahmoud Mohammed Taha kwa kosa la "uasi dhidi ya Uislamu". Miezi minne baadaye Nimeiry alipinduliwa kwenye mwaka huohuo.

Utawala wa Bashir

Sudan ilirudi kwa miaka michache chini yaserikali ya kiraia. Mapinduzi yaliyofuata mwaka1989 yalileta utawala wa jeneraliOmar al-Bashir. Vita ya wenyewe kwa wenye iliendelea hadi mwaka2005 ikamalizika kwaMapatano ya Naivasha baina ya Sudan naSPLA. Sudan Kusini ilipewa miaka hadi2011 kujitawala halafu kuwa na kura ya wananchi wa kusini kuhusu uhuru uliotangazwa mwaka uleule.

Tangu mwaka 2003 Bashir alisimamia pia vita ya jeshi lake nawanamgambo dhidi ya wakazi wasioWaarabu waDarfur waliopinga utawala wake.

Tarehe11 Aprili2019 Bashir alipinduliwa na jeshi lake baada yawiki kadhaa zamaandamano ya wananchi wa Khartum namiji mingine dhidi yake. Kupinduliwa kwake pamoja na kipindi chaserikali ya mpito ya kijeshi vilitangazwa na waziri wa ulinzi, jenerali Awad Mohammed Ibn Auf. Ilhali waandamanaji waliendelea kupinga serikali ya kijeshi, Ibn Auf alijiuzulu tarehe12 Aprili na siku iliyofuata, tarehe 13 Aprili, jeneraliAbdel Fattah Burhan alitangaza wanajeshi wanatafuta ushirikiano wa karibu na wapinzani wa utawala wa awali[1].

Watu na makabila

Kadiri yasensa za mwaka2008, wakazi walihesabiwa kuwa zaidi yamilioni 21.6.

Kadirio ni kwamba wakazi ni karibumilioni 48 mwaka2022.

Umma wa miji kama Khartoum (pamoja naOmdurman, na Khartoum ya kaskazini) waongezeka zaidi: umma wa miji hiyo yakadiriwa milioni 6-7 na wengine wahamiaji milioni 2 ambao wamekimbia vita vya kusini, magharibi, mashariki na pia wengine kwa sababu yaukame.

Sudan ina aina mbili zautamaduniWaafrika walio na Uarabu na Waafrika wasio Waarabu — namaelfu yamakabila na migao ya kabila,lugha tofautitofauti kwa makundi au kabila – migawanyiko hii uleta siasa za utengo naubaguzi.

Majimbo ya Kaskazini hasa ndio makubwa nchini Sudan, na pia miji mikubwa iko katika majimbo haya. Zaidi ya milioni 22 wanaoishi katika majimbo haya ni Waislamu-Waarabu na wanaongeaKiarabu, lakini wengi pia huongealugha 70 za kikabila hasaKinubi,Kibeja,Kifur,Kinuban,Kiingessana, kwa kikundi hiki kuna wale wavutia zaidi kama: Wa-Kababish kutoka Kordofan kaskazini, watu hawa wanaofugangamia; Ga’alin (الجعلين), Rubatab (الرباطاب),Manasir (المناصير) and Shaiqiyah (الشايقيّة); makabila ambao makao yao ni karibu na mito ni kama Baggara waKurdufan naDarfur; WakihamBeja eneo ya bahari ya Shamu na Wanubi wa Nile kaskazini, ambao wengine wamehamishwa karibu na mto Atbara. Eneo la Shokrya kwa Wabutana, Wabataheen wamepakana na Waga’alin na Washorya, upande wa kusini-magharibi eneo ya Butana. Pia kuna Warufaa, Wahalaween na makabila mengine mingi eneo la Gazeera na kwa ufuo wa Bluu Nile na eneo ya Dindir. Hata Wanubi kusini mwa eneo la Kurdufan na Wafur upande wa magharibi.

Makabila makuu

Lugha

Nchini Sudan kuna lugha zaidi ya 70. Kati yake, muhimu zaidi niKiarabu, ambacho ndicholugha rasmi pamoja naKiingereza. (AngaliaOrodha ya lugha za Sudan.)

Dini

Dini kubwa zaidi nchini niUislamu (97%).

Wakristo ni hasaWaorthodoksi wa Mashariki (Wakopti,Waethiopia naWaeritrea, lakini piaWaarmenia), halafuWaorthodoksi,Wakatoliki naWaprotestanti.

Elimu

Vyuo Vikuu vya Sudan ni kama vile:

Tazama pia

Marejeo

Tanbihi

  1. Kiongozi wa baraza la kijeshi la mpito nchini Sudan ameapakuung'oa utawala, BBC News Swahili 13-04-2019

Vitabu

Makala

  • "Quo Vadis bilad as-Sudan? The Contemporary Framework for a National Interim Constitution".Law in Africa (Cologne; 2005). Vol. 8, pp.  63–82.

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Serikali

Maarifa ya kawaida

Habari

Picha

Utalii

Mengineyo


Nchi zaAfrikaBara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) |Afrika Kusini |Algeria |Angola |Benin |Botswana |Burkina Faso |Burundi |Cabo Verde |Chad |Cote d'Ivoire |Eritrea |Eswatini |Ethiopia |Gabon |Gambia |Ghana |Guinea |Guinea Bisau |Guinea ya Ikweta |Jibuti |Kamerun |Kenya |Komori |Kongo (Jamhuri ya) |Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) |Lesotho |Liberia |Libya |Madagaska |Malawi |Mali |Misri |Morisi (Visiwa vya) |Mauritania |Moroko |Msumbiji |Namibia |Niger |Nigeria |Rwanda |Sahara ya Magharibi |Sao Tome na Principe |Senegal |Shelisheli |Sierra Leone |Somalia |Sudan |Sudan Kusini |Tanzania |Togo |Tunisia |Uganda |Zambia |Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje yaAfrika
Hispania:Kanari·Ceuta·Melilla |Italia:Pantelleria·Pelagie |Ufaransa:Mayotte·Réunion |Uingereza:·St. Helena·Diego Garcia |Ureno:Madeira
Makala hii kuhusu maeneo yaAfrika bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuSudan kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Sudan&oldid=1443388"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp