Stefania Turkewich-Lukianovych |
---|

|
Maelezo ya awali |
---|
Jina la kuzaliwa | Stefania Turkewich |
---|
Amezaliwa | 25 aprili 1898 |
---|
Asili yake | Lviv |
---|
Amekufa | 8 aprili 1977 |
---|
Aina ya muziki | Muziki wa Klasiki |
---|
Kazi yake | Mpiga piano, Mtaalamu wa Muziki, Mwalimu wa piano |
---|
Stefania Turkewich-Lukianovych (25 Aprili1898 – 8 Aprili1977) alikuwamtunzi wa muziki,mpiga piano namtaalamu wamuziki kutokaUkraina. Alikuwa mtunzi wa kike wa kwanza wa muziki wa Ukraina[1]. Matungo yake yalipigwa marufuku kwenye Ukraina namamlaka yaUmoja wa Kisovyeti.
Stefania alizaliwa hukoLviv, uliokuwamji waAustria-Hungaria wakati ule lakini sasa uko Ukrainia.Babu yake (Lev Turkevich) nababa yake (Ivan Turkevich) walikuwamakuhani.Mama yake, Sofia Kormoshiv (Кормошів), alikuwa mpiga piano[2].Familia nzima ilikuwa ya muziki na kila mtu alichezaala. Stefania alichezapiano,kinubi nakinanda cha matete (harmonium).
Kabla na baada yaVita Kuu ya Kwanza ya Dunia alisoma piano nanadharia ya muziki kwa wanamuziki kadhaa, hivi karibuni katika Chuo Kikuu na Chuo cha Muziki vya Lviv[2]: 10 . Alitunga kazi yake ya kwanza ya muziki mwaka wa 1919: Liturjia, ambayo ilifanywa mara kadhaa katikaKanisa Kuu la St. George[3]. Mwaka 1921, alisoma katika Chuo Kikuu chaVienna na Chuo Kikuu cha Muziki na Sanaa ya Maonyesho Vienna, ambapo alihitimu mnamo 1923 na Diploma ya Ualimu[3]. Miaka 1930-1934, alisoma katika Chuo Kikuu cha Charles hukoPraha na katika Chuo cha Muziki cha Praha, na hatimaye akapokea udaktari wake wa somo la muziki katika Chuo Kikuu Huru cha Kiukraina.Tasnifu yake ilikuwa juu ya mada yaHadithi za Kiukraina katika opera zaKirusi. Alikuwa mwanamke wa kwanza wa Kiukraina kupokea Ph.D.
Wakati waVita Kuu ya Pili ya Dunia aliendelea kufanya kazi huko Lviv, kwanza chini ya Sovyeti na kisha chini yaNazi. Baada ya vita, mnamo 1946, alikimbiawakomunisti na kuhamiaItalia, ambapo mume wake wa pili anafanya kazi kwaWaingereza. Baadaye mwaka huo huo, walihamia Uingereza, ambako aliishi hadi kifo chake mwaka wa 1977.
- Simfonia Nr. 1, 1937
- Simfonia Nr. 2a, 1952
- Simfonia Nr. 2b, toleo la pili
- Simfonieta, 1956
- Michoro Mitatu ya Kisimfonia, 1975
- Shairi la Kisimfonia "La Vita"
- Simfonia ya Anga-nje, 1972
- Suite kwa okestra mbili za ala za nyuzi
- Fantasia kwa okestra mbili za ala za nyuzi
- Msichana Wenye Mikono Iliyodhoofika, Bristol, 1957
- Mkufu
- Majira ya Kuchipua (Baleti ya watoto), 1934-1935
- Mavka - Nimfi wa Msitu, 1964-1967, Belfast
- The Scarecrow, 1976
- Mavka (isiyomalizika) inategemea Wimbo wa Msitu wa Lesia Ukrainka
- Tsar Okh au Moyo wa Oksana, 1960
- Ibilisi Kijana
- Kitalu cha mboga, 1969
- Liturjia, 1919
- Zaburi kwa Scheptytsky
- Kabla ya Vita
- Michoro mitatu
- Tumbuizo (Ah, hakuna paka) 1946
- Sonata kwa fidla na piano, 1935
- Kwarteti ya ala za nyuzi, 1960 - 1970
- Trio ya fidla, viola na chelo, 1960 - 1970
- Kwinteti ya piano, 1960 - 1970
- Trio ya ala za pumzi, 1972
- Mabadilifu ya Mada ya Kiukraina, 1932
- Fantasia. Suite kwa Piano inayotegemea Mada za Kiukraina, 1940
- Impromptu, 1962
- Grotesque, 1964
- Suite yaMlima, 1966 - 1968
- Mzunguko wa Nyimbo kwa Watoto, 1936-1946
- Nyimbo za Krismasi za Kiukraina na Shtchedrivka
- Habari njema
- Krismasi na Mchekeshaji, 1971
- Moyo, kwa mwimbaji mmoja na okestra
- Lorelei, Msimulizi, Kinanda cha matete na Piano, 1919. Matini ya Lesia Ukrainka
- Mei, 1912
- Mada za Nyimbo za Wenyeji
- Uwanja wa Uhuru - Wimbo kwa piano
- Wimbo wa Lemky kwa mwimbaji na ala za nyuzi