Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Soya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Soya
(Glycine max)
Soya
Soya
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:Planta (mimea)
(bila tabaka):Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka):Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka):Rosids (Mimea kamamwaridi)
Oda:Fabales (Mimea kamamharagwe)
Familia:Fabaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mharagwe)
Jenasi:Glycine
Willd.
Spishi:G. max
(L.)Merr.

Soya ni aina yamaharagwe nambegu zamsoya (Glycine max) katikafamiliaFabaceae.Asili yake ikoAsia ya Mashariki.

Nizao lamafuta nasifa yake ya pekee ni kiasi kikubwa chaprotini katika mbegu zake (40-50%). Kutokana nalishe yake kubwakilimo chake kimeeneaduniani. Kwawatu wasiokulanyama, mafuta ya soya na vyakula vinavyotokana na soya yana mahitaji yote ya protini kwagharama ndogo.

Rangi ya mbegu zake huwa ninjano,nyeupe lakini kuna pia aina zakahawia.

Utangulizi

[hariri |hariri chanzo]

Mmea huu ulitumika sana huko Asia ya Mashariki kwa zaidi ya miaka 5000. Tangukarne ya 1 KK ilikuwa zao la chakula muhimu sana katikaChina.

Katikakarne ya 18BK soya ilipelekwaUlaya ila haikutumiwa sana. Lakini baada ya kulimwaMarekani ilionekana kuletamavuno mazuri katikatabianchi hiyo. Iliendelea kuwa zao lenye kiwango kikuu cha mafuta na protini na kuwa na mavuno mazuri ya mara kwa mara.

Soya huwa na kiasi kikubwa cha asidi za phtyic, alpha-Linoplenic na daidzein. Bidhaa za soya kama vile TVP (textured vegetable protein), kwa mfano, ni muhimu sana kama viungo vya mapishi mengi ya nyama na maziwa.

Mafuta ya soya hutumika kwa namna mbalimbali. Wazalishaji wakuu wa soya ni Marekani,Brazili,Ajentina, China naIndia.

Mimea ya soya ikiwa shambani.
Maua madogo ya soya.
Aina za soya.

Aina za soya

[hariri |hariri chanzo]

Aina za soya hutofautiana katika ukuaji[[]],tabia nakimo. Huweza kukua chini yasentimita 20 lakini pia huweza kukua hata zaidi yamita 2.

Makaka ya soya,shina namajani hufunikwa navinyweleo vya kahawia. Majani hugawanyika katika sehemu kuu tatu, huku kila jani likiwa naurefu wa sentimita 6 – 15 naupana wa sentimita 2. Majani huanguka kabla ya kukomaa kwa mbegu. Maua, yenye uwezo wa kujichavusha yenyewe, hukua katikati ya majani na huwa na rangi yapinki,hudhurungi au nyeupe.

Tunda lake ni ganda lenye vinyweleo, ambalo hukua kwenye makundi ya maganda 3 – 5, huku kila ganda likiwa na ukubwa wa sentimita 3 – 8, na kuwa na mbegu 2 – 4 ndani yake, zenyekipenyo chamilimita 5 – 11.

Soya huja katika rangi mbalimbali, na mara nyingi katika rangi nyeusi, kahawia, bluu, njano, kijani na mchanganyiko wa rangi mbalimbali. Mbegu zilizokomaa ni ngumu, zisizopenyesha maji kwa urahisi hivyo kulinda kotiledoni na haipokotaili au kiini visiharibiwe. Kama gamba la nje la mbegu likiharibiwa, mbegu haitaota. Kovu linaloonekana kwenye mgegu hitwa hilamu, na katika mwisho mmoja wa hilamu kuna tundu dogo maalumu kwa kupitisha hewa na maji kwaajili ya kuchipua.

Kwa uthibitisho, mbegu za jamii ya mikunde, soya ikiwa miongoni mwao, huwa na aina ya protini ambayo hudumu hata baada ya kusharabu maji. A. Carl Leopold, alitafiti juu ya uwezo huu. Aligundua pia kuwa soya ina kiasi kikubwa cha kabohaidreti kinacholinda uhai wake.

Kwa pamoja, mafuta na protini vinafanya karibu 60% ya soya kavu kwa uzito; protini ikiwa 40% na mafuta 20%. Sehemu iliyobaki ni 35% kabohaidreti na 5% madini mengine mchanganyiko.

Virutubishi

[hariri |hariri chanzo]

Kwa matumizi ya binadamu, soya ni chanzo cha kiaminika cha protini iliyokamilika. Na soya huwa na humeng’enywa vyema kama ikipikwa kabla ya kuliwa. Kulingana na tafiti nyingi, bidhaa za soya zimeonekana kuwa na kiwango chaprotini cite kinachotakiwa tofauti na mimea mingine, soya huwa na protini inayoweza hata kuwa badala ya ile inayopatikana kwanyama, ambayo huwa na mchanganyiko wa mafuta mengi, hivyo kuipa soya alama za juu sababu haina mafuta hayo yanayoweza kuwa hatari kwa mwili wa binadamu.

Hata hivyo, licha ya faida nyingi za kiafya bado kuna mjadala mkubwa juu ya faida za kiafya za soya katika mlo.

Picha

[hariri |hariri chanzo]
  • Majani
    Majani
  • Maua
    Maua
  • Ua
    Ua
  • Makaka mabichi
    Makaka mabichi
  • Makaka mabivu
    Makaka mabivu
  • Soya
    Soya
  • Jibini ya soya (sheese)
    Jibini ya soya (sheese)
  • Soya zilizobanikwa
    Soya zilizobanikwa
  • Mafuta ya soya
    Mafuta ya soya
  • Unga wa soya
    Unga wa soya

Viungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]

Hasara za kilimo cha Soya

[hariri |hariri chanzo]

Upishi wa soya

[hariri |hariri chanzo]
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Soya&oldid=1377383"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp