Daudi alimchagua kuwa mrithi wake kwa sababu alikuwa uthibitisho hai wamsamaha aliopewa naMungu kwakuzini na hatimaye kumuua Uria.
Ufalme wake ulitazamwa naWayahudi kuwa na ustawi usio na mfano, kutokana nahekima yake naamani iliyopatikana wakati wote wa utawala wake.
Ufalme wake uliweza kustawi kuliko ule wa baba yake kutokana na msingi imara aliouweka Daudi. Lakini mwenyewe aliudhoofisha na kusababisha mara baada ya kifo chake utokee utengano kati ya makabila ya Kaskazini na yale ya Kusini.
Kati ya kazi muhimu alizozifanya, mojawapo ni kujengahekalu la Yerusalemu na kuliweka wakfu kwa sherehe kubwa ya siku saba, ambapo Mungu alionyesha kibali chake kwa kulijaza kwa sura ya wingu (1Fal 8). Polepolehekalu hilo likaja kuwa la pekee hatapatakatifu pengine pote pakakatazwa chini ya mfalmeYosia.
Ingawa Solomoni anasifiwa kwahekima yake, alishindwa kukwepamajivuno natamaa, akataka kuwapendeza wake zake waliokuwa 700 (mbali na masuria 300), wengi waoWapagani, hata akawajengea mahali pa kuabudia miungu yao akamchukiza Mungu hata akamtabiria mtoto wake atanyang’anywa sehemu kubwa ya ufalme (1Fal 11:1-13) ikawa hivyo.
Hata hivyo mwishoni aliweza kulaumiwa kwa kuzidisha fahari, hasa upande wa wanawake waliomvuta kwenda kinyume chaimani yaMungu pekee.
"Nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili niwahukumu watu wako,na kupambanua mema na mabaya;maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi"? (1Fal 3:9)
"Ee Bwana, Mungu wa Israeli, hakuna Mungu kama wewe,mbinguni juu wala duniani chini!Ushikaye maagano na rehema kwa watumishi wako,waendao mbele zako kwa mioyo yao yote". (1Fal 8:23)
Thomas E. Levy & Thomas Higham (eds.) (mhr.).The Bible and Radiocarbon Dating: Archaeology, Text and Science. London ;Oakville, CT.: Equinox Publishing (UK).ISBN978-1-84553-056-3.OCLC60453952.{{cite book}}:|editor= has generic name (help);Unknown parameter|origdate= ignored (|orig-date= suggested) (help)
Dever, William G. (2001).What Did the Biblical Writers Know and When Did They Know It?: What Archaeology Can Tell Us about the Reality of Ancient Israel. Grand Rapids, Mich.:Eerdmans Pub.ISBN978-0-8028-4794-2.OCLC45487499.{{cite book}}:Cite has empty unknown parameter:|coauthors= (help);Unknown parameter|origmonth= ignored (help)CS1 maint: ref duplicates default (link)