Mwelekeo wa kituo (mgawanyiko kati ya usiku na mchana) inategemea msimu.
Solistasi (pia:solistisi, kutokaing.solstice[3]) ni jina la siku mbili katika mwaka ambako tofauti kati ya urefu wa mchana na usiku ni kubwa zaidi kuliko siku zingine. Hutokea mara mbili kwa mwaka.
Tarehe ya kwanza ni 20 au 21 Juni na ya pili ni tarehe 21 au 22 Desemba.
Watu wanaoishi sehemu za jirani na ikweta huwa hawatambui tofauti kati ya muda wa mchana na usiku, ila kadri wanavyoishi mbali zaidi upande wa kusini au kaskazini wa ikweta, tofauti huwa kubwa zaidi.
Kwa kawaida kuna tofauti kati ya urefu wa mchana na usiku isipokuwa kwenye ikweta. Karibu na ncha za Dunia muda wa usiku na mchana unaweza kuwa mrefu hadi karibu nusu mwaka lakini kwa kawaida kuna majira ya mchana mrefu na usiku mrefu zinazobadilishana polepole. Mwendo huu unatokea kinyume kwenye nusutufe mbili za Dunia yaani wakati mchana unarefuka kwenyenusutufe ya kaskazi usiku unarefuka kwenyenusutufe ya kusi.
Katika kanda za karibu na ikweta tofauti hizi hazionekani kirahisi lakini kwenye nusutufe za Dunia upande wa kusini na kaskazini ya ikweta zimetambuliwa tangu karne nyingi na zimekuwa siku muhimu kwa makadirio yakalenda mbalimbali.
Wakati wa solistasi yaJuni, Jua linafika mahali pa juu zaidi kwenye anga wakati wa adhuhuri kwa mtazamaji kwenyenusutufe ya kaskazi ya Dunia, baadaye inaanza kushuka yaani kuonekana chini zaidi angani wakati wa adhuhuri hadisikusare ya Septemba. Kwa hiyo njia yake angani ni ndefu na hivyo muda wa mchana ni mrefu. Siku hiyo hiyo ya solistasi yaJuni, Jua linafika mahali pa chini angani pawezekanavyo wakati wa adhuhuri kwa mtazamaji kwenyenusutufe ya kusini ya Dunia. Hapa njia yake angani ni fupi hivyo muda wa mchana ni mfupi. Kinyume chake muda wa usiku unabadilika kuwa mrefu au mfupi.
Vivyo hivyo wakati wa solistasi ya Desemba Jua linafika mahali pa juu kwenye anga wakati wa adhuhuri kwa mtazamaji kwenyenusutufe ya kusi ya Dunia, baadaye inaanza kushuka yaani kuonekana chini zaidi angani wakati wa adhuhuri hadisikusare ya Machi. Siku hiyo hiyo, Jua linafika mahali pa chini angani pawezekanavyo wakati wa adhuhuri kwa mtazamaji kwenyenusutufe ya kaskazi ya Dunia.