Slothi (kutokaKiing.:sloth) auwavivu-miti nimamalia wa ukubwa wastani wafamiliaCholoepodidae (slothi wenyevidole viwili) naBradypodidae (slothi wenye vidole vitatu) wanaoainishwa katikaspishi sita. Ni wana waodaPilosa na kwa hivyo huwa uhusiano naarmadilo nawalasisimizi walio nakucha sawa na zile za slothi. Spishi zinazopo hadu sasa huishimitini mwamisitu mizito yaAmerika ya Kati naya Kusini, na hujulikana kwa kusonga polepole, kwa hivyo walipewa jina la slothi ambalo kwa Kiingereza lina maana ya "mvivu", au kwaKiswahili mvivu-miti.
Nusuoda ya kitaksonomia ya slothi niFolivora, wakati mwingine inaitwaPhyllophaga. Majina mawili yanamaanisha "mla-majani"; kutokaKilatini naKigiriki. Majina yawanyama hawa yanayotumiwa na makabila yaEkwado niritto,rit naridette, ambayo humaanisha "kulala", "kula" na "mchafu" kutoka kabila yaWatagaeri waHuaorani.
Slothi wanaainishwa kama wala-majani kwa sababu hulamaua namajani kwa kawaida. Slothi wengine wenye vidole viwili hulawadudu,watambaazi wadogo nandege. Majani wanayoyakula hayawatolei nishati nyingi, kwa hivyo, slothi wanautumbo mkubwa.Slothi hawawezi kuishi nje yamisitu ya mvua ya kitropiki ya Amerika ya Kusini na ya Kati, katika mazingira hayo slothi ni viumbe wanaoishi vizuri.
Slothi mdogo
Slothi manyoya-marefu
Slothi koo-jeupe
Slothi kusi
Slothi kaskazi
 | Makala hii kuhusu"Slothi" inatumia neno (au maneno) ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio la kutafsiri neno (au maneno) la asilisloth kutoka lugha ya Kiingereza. Neno (au maneno) la jaribio nislothi. Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao kwenye ukurasa wa majadiliano ya makala.
Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.
|