Kabla ya kumilikiwa na Microsoft, Skype ilimilikiwa naeBay kuanziaSeptemba2005 hadi2011. eBay iliinunua kutoka kwa walioizindua kwadola zaKimarekanibilioni 2.6 miaka 2 baada ya kuzinduliwa.[1][2]
Mwaka wa2009, eBay iliuzia Silver Lake, Andreessen Horowitz, na Bodi la Mipango ya Uwekezaji wa Pensheni la Kanadaasilimia 65 yahisa za Skype kwa kima cha dola za Kimarekani bilioni 1.9 wakatithamani ya Skype ilikuwa takriban dola za Kimarekani 2.75.
Tarehe10 Mei2011, Microsoft ilianza mipango ya kumiliki Skype Communications, S.à r.l kwa kima cha dola za Kimarekani bilioni 8.5 na tarehe13 Oktoba mwaka huo mipango ya umiliki ikakamilika.[3][4]
Jina Skype linatokana na "Sky peer-to-peer" ambapo ilifupishwa kuwa "Skyper". Hata hivyo,anuani ya tovuti yenye jina hilo ilikuwa tayari imenunuliwa na kampuni nyingine,[5] hivyo herufu "r" iliondolewa na kuwa Skype.[6]
Makala hii kuhusu mambo yauchumi bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuSkype kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.