Skii asilia: Wasami katika Skandinavia wakati wa karne ya 18Aina mbalimbali ya skii zinazotumiwa mlimaniKuruka mbali kwa skiiSkii za mbio kwenye tambarare
Skii aurelitheluji niubao mrefu na mwembamba unaofungwa chini yakiatu kwa kusudi la kutelezea kwenyetheluji.
Vifaa hivi vilianzishwa namataifa yaliyoishi katikamazingira yabaridi ambako mara kwa mara uso wa nchi hufunikwa kwa theluji.
Ilhali theluji inaweza kufunika uso wa nchi kwaunene wasentimita au hatamita kadhaa si rahisi kutembea juu yake kwa sababumguu unaweza kuzama ndani ya theluji kwa kila hatua ambayo inachelewesha mwendo na kuchosha.
Kufunga skii mguuni kunaleta faida mbili:
uso mkubwa wa skii huzuia kuzama chini ndani ya theluji
uso nyororo wa skii unaruhusu kuteleza juu ya theluji kwa kasi kubwa kuliko kukimbia kwenye nchi kavu.
Asili ya jina "skii" iko katikaKinorwei cha kale.[1][2] Matamshi yake kwa kawaida ni "shi".
Mifano ya kale ya skii imepatikana kutokaUrusi,Uswidi naNorwei ambayoumri ulioweza kuthibitishwa watu walianza kutumia vifaa hivi miaka 8,000 iliyopita.
Teknolojia ya skii iliendelezwa mwanzoni makarne ya 20 katika nchi zaSkandinavia kwa shabaha ya kumwezesha mtumiaji kupigakona haraka zaidi.Maendeleo yalihusu hasa namna ya kufunga mguu kwenye ubao na pia matumizi yaplastiki badala ya ubao, pamoja na kubunimabuti ya pekee kwa matumizi pamoja na skii.
Mabadiliko hayo yaliendeshwa hasa nawanamichezo waliokuta skii kwa watumiaji wake wa kiasili na kuipeleka kwa nchi nyingine kwa kusudi laburudani namashindano.
Skii imeibuka kutoka kujengwa kwa ubao mgumu uliochongwa. Baada ya kuenea kwamichezo ya skii katikaUlaya ubao mgumu ulikuwa haba na ghali, hivyomafundi walianza kuunganisha aina mbalimbali za ubao.
Tangu kupatikana kwa plastikimata hii imetumiwa pia kwa kutengeneza skii. Kwa mashindano ya hali ya juu kuna pia skii zinazotengenezwa kwa kutumia teknolojia ya juu yakaboni.