Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Siku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mabadiliko ya siku husababishwa na mzunguko wa dunia yetu kwenye mhimili wake. Hapa tunatazama upande wa mchana unaoangazwa na jua. Upande mwingine ni upande wa giza au usiku.

Siku nimuda wasaa 24 ambamo tunaona vipindi viwili: kile chamwanga wamchana na kile chagiza lausiku.

Mchana na usiku

Mabadiliko hayo ya mchana na usiku husabibishwa na mzunguko wadunia kwenyemhimili wake. Upande wa dunia unaotazamajua unapata mwanga wa mchana lakini upande mwingine usiotazama jua unakuwa gizani.

Sisi pamoja navitu vyote vilivyo juu ya uso wa dunia, yaanibahari,mito,milima,binadamu,misitu,majangwa,majengo,barabara na kila kitu unachoweza kuwaza kuwa kipo kwenye uso wa dunia, basi vyote huwa katika mwendo kadiri dunia inavyojizungusha kwenye mhimili wake. Hivyo basi, wakati upande ule wa uso wa dunia tulipo unapogeukia au kutazamana na jua, basi kwetu inakuwa mchana, pale ambapo upande huo hatutazamani na dunia, basi tunapata usiku, yaani tunakuwa kwenye giza.

Mwanzo na mwisho

Mwanzo na mwisho wa siku ni jambo la mapatano baina ya watu ma hapa kuna kawaida tofautitofauti katikatamaduni za Dunia.

Uchumi nasheria siku hizi hufuatamuda sanifu wa dunia unaopanga mwisho na mwanzo wa siku yakalenda katikati ya usiku, yaani saa sita usiku, au kwalugha nyingine kwenye 24:00 au 0:00h.

Kalenda zakidini kamakalenda ya Kiyahudi naKalenda ya kiislamu hupanga mwisho wa siku wakati wamachweo, ambayo ni pia mwanzo wa siku mpya. Kwa sababu hiyosherehe yaSabato katikaUyahudi (ambayo inalingana naJumamosi yaKiswahili) inaanza baada ya machweo kwenyeIjumaa, na pia utaratibu wa kuzuiakazi unakwisha kwenyejioni ya Jumamosi baada ya machweo.

Muda wa siku

Mzunguko huo wa dunia kwenye mhimili wake unachukua muda wanukta (sekunde) 86,400 au masaa 24.

Kwa sababu muda wa mzunguko haulingani kikamilifu nakipimo cha sekunde kuna siku ndefu au fupi zinazopatikana kwa kuingiza au kupunguza nukta moja kufuatana na azimio yawataalamu wawakati. Hii haina umuhimu wowote katikamaisha ya kila siku lakini inapaswa kuangaliwa pale ambapo saa kamili sana yakiatomi hutumiwa.

Siku na mwaka

Dunia, pamoja na kujizungusha kwenye mhimili wake, ina mwendo mwingine pia , yaani ule wa kulizunguka jua. Ikikamilisha mwendo huu basimwaka unakuwa umekamilika. Kipindi cha mwaka hakilingani kwa kila mwaka: kuna miaka mirefu na miaka mifupi. Hii ni kwa mujibu waKalenda ya Gregori ambapo mwaka wa kawaida (mfupi) huwa na siku 365 na kila mwaka wa nne (mwaka mrefu) kuwa na siku 366.

Alfajiri huko Taritari, Nueva Esparta, VenezuelaVipindi vyasikuKutwa huko Knysna, Afrika Kusini

UsikuUsiku katiUsiku wa mananeAlfajiriPambazukoAsubuhiAdhuhuriMchanaAlasiriJioniMachweo

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Siku&oldid=1051598"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp