Maziwa yang'ombe, lakini pia yawanyama wengine, huwa na kiasi cha shahamu ndani yake. Kama maziwa yanakaa baada ya kukamuliwa, shahamu inapanda juu na kuonekana kwenye uso wake. Hapo inaweza kukusanywa.
Siagi ni thabiti kama inatunzwa katikajokofu, lakini nje yake inalainika na kuyeyuka kabisa, kuwa kama mafuta mnamosentigredi 30-35.[1]
Siagi inaharibika haraka katikatabianchi yajoto pasipo jokofu, hivyo matumizi yake kama chakula cha pekee, tofauti na maziwa, yalianza katika nchi zenye tabianchibaridi.[2]Mataifa ya kale walitumia siagi mara nyingi kamadawa la kupakaa.
Siagi inatengenezwa kwa kutisikisha maziwa nakazi hii inarahisishia kutengana kwa shahamu na sehemu nyingine.Krimu inayokusanyika kwenye uso wake bado niemalshani ya shahamu namaji inayoendelea kukandamizwa kwa shabaha ya kupunguza maji ndani yake. Wakati siagi imekuwa tayari inaasilimia 15-20 za maji ndani yake.
Zamani siagi ilitengenezwa kwamikono. Tangukarne ya 19mbinu mbalimbali ziligunduliwa kwa kutengeneza siagikiwandani. Siagi hii inafikasokoni mara nyingi ikitiliwa tayari kiasi chachumvi.
Tangu karne ya 19majarini ilibuniwa katikaUlaya kama chakula mbadala kwa sababu wakazimaskini kwenyemiji iliyokua haraka walikosa uwezo wa kununua siagi. Majarini hutengenezwa kutoka mafuta yamimea (k.v.alizeti,karanga,mawese) pamoja na maji nagharama zake ni nafuu kuliko siagi.
KuleUhindi katikamazingira ya joto watu walibuni njia ya kutunza siagi kwamuda mrefu kwa njia ya kuichemsha hadi maji yote ndani yake yatoke nje. Tokeo lake huitwa ghee (tamka: gii): namna hiyo ya siagi inaweza kutunzwasiku nyingi bila jokofu. Hadi leo ghee ni sehemu muhimu yaupishi wa Kihindi.
↑Mwandishi wa Roma ya Kale Plinius Mzee alitaja siagi kuwa chakula cha "washenzi wa kaskazini" tazamaCHAP. 35.—TWENTY-FIVE REMEDIES DERIVED FROM BUTTER, ktk Pliny the Elder, The Natural History John Bostock, M.D., F.R.S., H.T. Riley, Esq., B.A., Ed.