Elimu ya sekondari (shule za upili), katika mifumo ya kisasa yaelimuulimwenguni, huchukua kipindi cha pili chaelimu rasmi ambayo hutokea wakati waujana wawanafunzi.
Mfumo huu hutofautiana na masomo ya msingi ambayo ni ya lazima, ni ya jumla na yanayofanana. Yale ya shule za upili ni teule na ya hiari. Shule hizi hujulikana kama sekondari, shule za upili, shule za kati, vyuo au shule za ujuzi wa kitaalamu kulingana na kipindi au mfumo unaofuatwa.
Maana ya dhana hizi hutofautiana kutoka mfumo mmoja hadi mwingine. Mpaka kamili kati yaelimu ya msingi na ya upili hutofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine. Tofauti hizi zipo hata katika nchi, lakini kwa jumla hutokea kati yamwaka wasaba na wakumi wa kusoma.
Elimu ya sekondari hutokea katikaumri wa ujana. NchiniMarekani naKanada, elimu ya msingi na sekondari kwa pamoja hurejelewa kama elimu ya K-12 na nchiniNyuzilandi, elimu hii hurejelewa kama elimu ya miaka 1-13. Azma ya elimu ya sekondari ni kutoa maarifa ya kawaida, kutayarisha wanafunzi kwaelimu ya juu au kuwafunzakazi moja kwa moja.
Tunapaswakujitahidi katika kuhamasisha elimu ya sekondari kwani huwezesha kufikiachuo kikuu.
Elimu ya sekondari iliibuka nchini Marekani mwaka1910 na ilisababishwa na kuwepo kwabiashara kubwa namaendeleo yateknolojiaviwandani. Ili kuafikia mahitaji ya kazi, shule za upili zilijengwa namtaala uliolenga maarifa ya kazi zaofisi na za sulubu ukazinduliwa. Hii ilibainika kuwa njia ya manufaa kwamwajiri kwani uimarishaji wahuduma za kibinadamu uliwafanya waajiriwa kuwa madhubuti kazini na kushushagharama kwa waajiri, huku waajiriwa wakinufaika namishahara minono ikilinganishwa na waliokuwa na elimu ya msingi pekee.