Shirika la A.H. Belo | |
---|---|
![]() | |
Jina la kampuni | Shirika la A.H. Belo |
Ilianzishwa | Dallas,Texas kutoka kampuni ya ,hapo awali, Belo |
Huduma zinazowasilishwa | Uchapishaji |
Mmiliki | Robert W. Decherd Mkurugenzi Mkuu Rais Mwenyekiti |
Aina ya kampuni | Kampuni ya Umma |
Makao Makuu ya kampuni | Dallas ,Texas![]() |
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii | Magazeti |
Nchi | Marekani |
Tovuti | http://www.ahbelo.com/ |
A.H Belo Corp ni kampuni inayohusika na vyombo vya habari iliyokuwa na makao yakeDallas,Marekani. Kampuni hii inamiliki magazeti manne ya kuchapishwa kila siku na majarida matano madogomadogo. Shirika la sasa liliundwa baada ya Shirika la Belo kugawanya operesheni zake za utangazaji na za uchapishaji kuwa mashirika mawili. Mkurugenzi mkuu ni Robert Decherd ambaye alikuwa akiongoza Shirika la Belo kabla ya mgawanyiko huo kufanyika. Makao makuu ya kampuni hii ni Jengo la Belo Building katika eneo laDallas.
Kampuni hii ilianzishwa kama shirika dogo lililomilikiwa na Shirika la Belo mnamo 1 Oktoba 2007. Mnamo 8 Februari 2008 hisa za kampuni ziliuzwa kwa umma ili watu wapate kumiliki kampuni hii. Ingawa kampuni hii ilianzishwa katika mwaka wa 2008, shirika hili lina mizizi yake na historia yake kutoka mwaka wa 1842. Shirika la Belo lilitumia jina la A.H. Belo kutoka mwaka wa 1926 hadi mwaka wa 2002 lilipofupishwa kuwa Belo. Mgawanyiko wa shirika hili liliwapa nafasi ya kutumia jina la zamani ambalo ni linatumika kwa makumbusho ya Alfred Horatio, mwanzilishi waDallas Morning News.
oAl Día (Lugha yaKihispania -Dallas,Texas)oQuick (gazeti la kila wiki la bure linalochapishwa naDallas Morning News -Dallas,Texas)
oBusiness Press (Riverside,California)oThe Difference Desert Daily (Riverside,California)oLa Prensa en Linea (Lugha ya Kihispania - Riverside, California)