Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Sherone Simpson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rekodi za medali
Riadha ya Wanawake
Anawakilisha nchi:Jamaika
Michezo yaOlimpiki
Dhahabu2004Athens4 x 100
Fedha2008Beijing100m
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya IAAF katika Riadha
Fedha2005Helsinki4x100 m
Michezo ya Jumuia ya Madola
Dhahabu2006Melbourne200 m
Dhahabu2006 Melbourne4 x 100 m

Sherone Simpson (alizaliwa12 Agosti1984) nimwanariadha wa nchi yaJamaika ambaye huiwakilisha nchi yake katika mashindano ya kimataifa. Alishinda medali ya dhahabu katika mbio ya 4 x 100m katika mashindano ya Olimpiki ya 2004 na medali yafedha katika Mashindano ya Mabingwa wa Dunia ya 2005.Alishinda medali ya fedha katika mbio ya 100m katika Olimpiki ya 2008 baada ya kukimbia kwa muda mmoja na mwenzake wa Jamaika ,Kerron Stewart. Muda wake wa kibinafsi wa 10.82 s katika mbio ya 100m,Simpson ndiye mwanariadha mwanamke wa nne bora nchini Jamaika.Mbele yake niMerlene Ottey,Shelly-Ann Fraser naKerron Stewart. Muda wake bora wa 22.00 s katika mbio ya 200m ndio muda wa nne bora katika orodha ya Jamaika akiwa nyuma yaMerlene Ottey,Grace Jacson,Juliet Cuthbert,Veronica Campbell-Brown naKerron Stewart. Amekimbia mbio ya 200m na muda huu mara mbili. Kocha wa Simpson ni Stephen Francis mjiniKingston.Jamaika, anaposoma katikaChuo Kikuu cha Teknolojia. Yeye ,pia, alisoma katika shule ya Manchester High.

Sherone Simpson(wa tatu kutoka kushoto) katika sherehe ya kutuzwa medali katika mbio zaOsaka za 2007,akiwa na wenzakeKerron Stewart naShelly-Ann Brooks

Wasifu

[hariri |hariri chanzo]

Simpson alishinda medali yadhahabu katika mbio ya wanawake ya 200 m katika Michezo ya Jumuia ya Madola ya 2006 , huku akishinda Veronica Campbell.Katika mbio hizo, Jamaika ilishinda medali za dhahabu kwa mbio za 100m na 200m. Jamaika ilishinda ,pia, medali zote za dhahabu katika mbio za kuruka viunzi.

Katika Olimpiki ya 2008 mjiniBeijing alishiriki katika mbio ya 100m. Katika mbio za mchujo,alikuwa wa tatu nyuma Yevgeniya Polyakova na Jade Bailey katika muda wa 11.48s na kuhitimu awamu ya pili. Katika awamu ya pili aliboresha muda wake ukawa 11.02s na kushinda mbele yaMuna Lee naChandra Sturrup. Katika mbio za nusu fainali alikuwa nambari ya nne na 11.11 s akapata nafsi katika fainali. Katika mbio za ajabu na wenzake wa Jamaika,Shelly-Ann Fraser na Kerron Stewart, walishinda medali huku Fraser akipata ya dhahabu na Stewart & Simpson wakipata ya fedha. Akiwa pamoja na Fraser,Stewart,Sheri-Ann Brooks,Aleen Bailey na Veronica Campbell-Brown alishiriki katika mbio ya 4 x 100. Katika mbio za mchujo(bila Simpson na Stewart) walikuwa wa kwanza mbele yaUrusi,Ujerumani naUchina. Muda wa sekunde 42.24 ndio uliokuwa bora kabisa kati ya mataifa 16. Kutokana na matokeo haya, walihitimu kushiriki katika mbio ya fainali.Katika fainali waliweka Simpson na Stewart badala ya Bailey na Brooks. Hatimaye,hawakumaliza mbio yao kutokana na makosa katika kubadilishana kijiti cha kumpa mwanariadha mwenzako. [14]

Ubora wa binafsi

[hariri |hariri chanzo]
ShindanoMudaUpepoPahaliTarehe
100 m10.82-0.7Kingston,Jamaika24 Juni 2006
200 m22.00-0.3Stockholm,Uswidi25 Julai 2006
+1.3Kingston,Jamaika25 Juni 2006
400 m51.25Kingston,Jamaika22 Machi 2008

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. Athlete biography: Sherone Simpson, beijing2008.cn,

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Alitanguliwa na
MarekaniAllyson Felix
Wanawake Bora wa Mwaka katika mbio ya 200m
2005
Akafuatiwa na
MarekaniAllyson Felix


Mabingwa wa Mbio za 100m za IAAF(Wanawake)

 1977: Marlies Göhr (GDR)  •  1979 – 1981: Evelyn Ashford (Marekani)  •  1985: Marlies Göhr (GDR)  •  1989: Sheila Echols (Marekani)  •  1992: Natalya Voronova (Urusi)  •  1994: Irina Privalova (Urusi)  •  1998: Marion Jones (Marekani)  •  2002: Tayna Lawrence (Jamaika)  •  2006: Sherone Simpson (Jamaika)

Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Sherone_Simpson&oldid=1244294"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp