Serbia (kwaKiserbokroatia: Република Србија au Republika Srbija) ni nchi yaUlaya kwenyerasi yaBalkani.
Imepakana naHungaria,Bulgaria,Romania,Masedonia Kaskazini,Kosovo (auAlbania),Montenegro,Bosnia na Herzegovina naKroatia.
Nchi ni mwanachama waUmoja wa Mataifa na inatarajia kujiunga naUmoja wa Ulaya.
Mji mkuu niBelgrad, wenye wakazimilioni 1,2.
Miji mingine muhimu niNovi Sad (mji mkuu wajimbo linalojiendesha laVojvodina),Niš (mji mkubwa zaidi wa kusini na mashariki mwa Serbia) naKragujevac katika Serbia sahihi,Priština katika jimbo linalojiendesha la Kosovo (hali si ya uhakika).
Miji mingine mikubwa niSubotica,Novi Pazar,Pančevo,Zrenjanin,Kraljevo,Kruševac,Leskovac,Smederevo na mingine.
Miji muhimu kihistoria na kiutamaduni (ingawa midogo) niSremski Karlovci,Negotin,Vranje,Zaječar naPožarevac.
Waslavi walihamiaBalkani baada yakarne ya 6.
Kati yao, Waserbia waliundafalme mbalimbali mwanzoni mwaKarne za Kati.
Mwaka1217Ufalme wa Serbia ulitambuliwa naRoma naBizanti na mwaka1346 ulifikiakilele chaustawi wake kamaDola la Serbia.
Hali hiyo haikudumumuda mrefu, tena katikati yakarne ya 16 eneo lote la Serbia ya leo lilitekwa naWaosmani, ingawa wakati mwingine sehemu yake ilitawaliwa naDola la Wahabsburg.
Mwanzoni mwakarne ya 19,mapinduzi ya Serbia ililetaufalme wa kikatiba wa kwanza katika Balkani.
Ufalme huo ulizidi kuenea na baada yavita vikuu vya kwanza vilivyosababishavifo vingi vyaraia zake, Serbia iliungana namakabila kuanzishaYugoslavia iliyodumu hadimiaka ya 1990 iliposambaratika kwavita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mwaka2006 hataMontenegro ilitengana na Serbia, ila kwaamani.
Mwaka2008bunge lajimbo laKosovo lilijitangaziauhuru.
Nchi, ukiondoa Kosovo, ina wakazi 7,186,862 kwenye eneo lakm² 88.361. Wengi wao wana asili yaKislavoni.
Upande wadini 85% niWaorthodoksi, 5%Wakatoliki, 3%Waislamu, 1%Waprotestanti.
|
---|
Nchi huru | |
---|
Nchi zisizokubaliwa na umma wa kimataifa | |
---|
Maeneo yanayojitawala chini ya nchi nyingine | |
---|
|
 | Makala hii kuhusu maeneo yaUlaya bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuSerbia kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |