Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Sayansi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Galileo Galilei, baba wa sayansi ya kisasa.[1]:Vol. 24,No. 1,p. 36

Sayansi nimaarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli ambazo zimebainishwa hazijathibitishwa.[2]

Mara nyingiGalileo Galilei anahesabiwa kuwababa wa sayansi ya kisasa.

Aina za sayansi

Mtu aliyerushwa hadi angani. Kufikia katikati yakarne ya 20binadamu ameweza kukua kisayansi na hivyo kuvumbuateknolojia zilizomwezesha kuruka na kuelea katika anga la juu kabisa laDunia kwa mara ya kwanza na kuchunguzaanga-nje.

Kuna sayansi mbalimbali ambazo huainishwa katika makundi yafuatayo:

Sayansi Asili k.m.

Sayansi Umbile k.m.

Sayansi Jamii k.m.

Sayansi Tumizi k.m.

Pia, kuna sayansi zinazohusu mada maalumu mbalimbali:

Mbinu za kisayansi

Charles Darwinmwaka1854, alipokuwa anatungakitabu chake "On the Origin of Species".

Msingi wa sayansi ni vitendo. Vitendo vya kisayansi vina njia zake zinazotumika kuthibitisha kweli fulani.

Namna ya kueleza jambo kisayansi huchimbuka tokanadharia ama udhanifu. Halafu, ili kweli ikubalike, hutoka kwenye udhanifu na kwa kupitiamajaribio rasmi, hutengenezadhana kamili ama nadharia kama ni shauri la kueleza mwenendo natabia.

Hivyo,asili ya njia ya kisayansi nimtazamo unaokwenda sambamba na vitendo vinavyochunguzwa. Kutoka mitazamowanasayansi wanaunda nadharia. Baadaye wanaangalia kama bashiri za nadharia ni kweli. Zisipokuwa kweli watakanusha nadharia hiyo. Ikionekana kwamba mara nyingi sana nadharia ilibashiriukweli, na haijakosea, itakuwa nadharia inayokubalika.

Sura ya kisayansi

Mara chache, maarifa yatokanayo na sayansi yanaweza kupinga hali ya kawaida. Kwa mfano nadharia yaatomu inasema kwamba katikajiwe (maada yabisi) kunauvungu (dutu tupu), na kwamba atomi zinacheza katika nafasi ndogo katika jiwe ukifananisha namaada kimiminika. Lakini kwa nadharia hii tunaweza kueleza mambo mengi, hata kwa nini tunaweza kusema kwamba jiwe halina uvungu.

Historia

Aristotle (384 KK322 KK) alichangia ukuaji wa sayansi.

Sura ya kiutamaduni

Sayansi iliaanza kamaudadisi wa mtu mmojammoja; lakini kadiri maarifa yanavyopanuka, inakuwa vigumu kwa mtu mmoja kufanya mchango wa kujitenga. Hivyojumuiya zimebeba kusudi ambalo hapo mwanzo lilionekana kama ni shauku la mtu mmojammoja kama awali.

Hii hufanya mkururo waugunduzi amauvumbuzi kuwa sehemu yahistoria ya sayansi.Majina nasifa hutajwa sambamba na shauri la aliyepelekea.

Sayansi najamii huenda pamoja katika kuleta mabadiliko, kwa kuwa mabadiliko huletwa na watu wenyewe.

Sayansi na siasa za dunia

Picha ya dunia ikionyesha kutokea kwamabara tangu kugawanyika kwaPangea mpaka hivi leo.

Katikadunia hii ya leo,maendeleo ya watu hujidhihirisha sana kutokana na jinsi jamii husika ilivyopiga teke katika uwanja huu.

Ingawaje haibainishwi wazi miongoni mwa sura ya mambo ya kidunia, sayansi kwa kweli ninguvu inayoweza kubadilimaisha ya watu kwa wema; lakini katikakilele chake cha mafanikio, vyombo vyenye nguvu zamamlaka nafedha hushikilia baadhi yamatunda yake katika hali yakibiashara nakiutawala zaidi.

Sayansi na maendeleo

Mambo mbalimbali ya kikemikali yaliyosomwa naMichael Faraday na kuripotiwa katikakitabuHistoria ya kikemikali ya mshumaamwaka1861.

Wapo watu pia ambao hutumia sayansi kujaribu kuboresha maisha ya watu wote kwa ujumla. Hivyo sayansi haibakii tumikononi mwa wenye kushika dau kimifumo, bali changamoto ya wote wenye kutaka kuleta maendeleo ya ujumla.

Hivyo roho ya uchunguzi ndiyo iliyoleta kuzaliwa, kukua na kutapakaa kwa sayansi.

Tazama pia

Tanbihi

  1. "Galileo and the Birth of Modern Science".American Heritage of Invention and Technology.24.
  2. Ufafanuzi katikaKamusi ya Kiswahili Sanifu: "sayansi /sajansi/ nm (-) [i—] elimu inayotokana na uchunguzi, majaribio, vipimo na kuthibitishwa kwa muda uliopo. "Ufafanuzi katikaKamusi Kuu: "sayansi - tawi la maarifa linalohusu nadharia, vipimo, uchunguzi wa hatua kwa hatua na uthibitishaji wa kuwepo au kutokuwepo kwa kitu au jambo katika hali halisi "
Sayansi portal
Sayansi asili
Sayansi umbile
Sayansi ya jamii
Sayansi tumizi
Sayansi za dunia
Makala hii kuhusu mambo yasayansi bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuSayansi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Sayansi&oldid=1233832"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp