Waislamu wanapaswa kufunga chakula nakinywaji, yakiwemomaji, kuanziaalfajiri hadimagharibimwezi mzima waRamadhani. Saumu za sunna ni saumu yoyote ambayo si ya lazima, ila mtu anaifunga ili kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.
Saumu ina fadhila kubwa sana, na thawabu nyingi mno, tena maradufu, na kwa hakika Mwenyezi Mungu ameinasibisha saumu kwake yeye kwa ajili ya kuipa utukufu na kuitukuza. KatikaHadithi Al-Qudsy iliyopokewa na swahaba Abu Hurayrah, anasema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu: “kila tendo la mwanadamu huongezwa malipo ya wema wake mara kumi ya mfano wa jema hilo alilolitenda mpaka hufikia kuongezwa (huku kwa malipo ya wema huo) hadi nyogeza mara sabiini. Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Isipokuwa saumu, kwani hiyo saumu ni yangu mimi, na mimi ndiye mwenye kutoa malipo yake; (mja wangu) anaacha matamanio yake na chakula chake kwa ajili yangu. Katika kufunga saumu kuna furaha mbili: furaha (ya kwanza) ni pale anapofungua saumu aliyefunga, na furaha (ya pili) ni wakati (aliyefunga) atakapokutana na Mola wake. Na harufu inayotoka kwenye kinywa cha aliyefunga ni nzuri sana mbele ya Mwenyezi Mungu kushinda harufu ya miski”.[Imepokewa na Bukhari na Muslim.]<[2]
Baadhi ya fadhila za saumu katika Uislamu: "Asema Mwenyezi Mungu: Enyi mloamini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andkikwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kucha mungu.(Mfunge) siku maalumu za kuhisabika.na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimiza hisabu katika siku nyingine. Na wale wasio weza watoe fidiya kwa kumlisha masikini na atakaye fanya wema kwa kujitolea, Basi ni bora kwake na Mkifunga ni bora kwenu kama mnajua".(Al-Baqarah- Aya 183: 185)[3]
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.