Picha ya eksirei inayoonyeshakivuli cha kansa katika mapafu.
Saratani(kutokaKiarabu سرطان,sartan) aukansa (kutokaKiingerezacancer) ni aina zaugonjwa unaotokana naseli zamwili zinazoanza kujigawa yaani kukua bila utaratibu na bila mwisho.
Ukuaji huu unaleta uvimbe mwilini unaozidi kuwa mkubwa hadi unabanaviungo vya mwili kamaneva,mishipa ya damu,ubongo,mapafu,maini,utumbo na kadhalika na hivyo kuzuia visifanye kazi. Hivyo inasababishakifo, mara nyingi baada ya kipindi chamaumivu makali.
Pamoja na hayo kansa / saratani huwa natabia za kujisambaza mwilini mahali pengi baada yamuda fulani na kusababisha kutokea kwa vimbe nyingi mwilini vinavyoendelea kukua hovyo. Kama uvimbe hauna uwezo wa kusambaza seli zake mwilini na kusababisha vimbe mpya si saratani.
Kansa inaweza kutokea kwamtu yeyote lakini hutokea zaidi kwa watu wenyeumri mkubwa na watu wanaoathiriwa nakemikali mbalimbali. Katikanchi zilizoendelea ambako wanachi hufikia umri mkubwa saratani iko kati ya sababu kuu zakifo.
Hali nzuri yalishe na mtindo bora wamaisha ni kigezo muhimu sana katika kuzuia saratani[2] na pia ni sehemu muhimu ya matibabu na kudumisha maisha bora baada ya matibabu ya saratani kumalizika.
Matumizi ya baadhi yavyakula huweza kuongeza uwezekano wa kupata baadhi yasaratani na vyakula vingine huweza kupunguza uwezekano wa kupata saratani.
Uzito wa mwiliunapozidi kiasi unaweza pia kuongeza uwezekano wa kupata baadhi ya saratani.
Pamoja na mtindo bora wa maisha unaodumisha ulaji bora,mazoezi ya mwili,uzazi naunyonyeshaji wawatoto wachanga, ni muhimu pia kupata na kufuataushauri wa wataalamu waafya kuhusuupimaji unaoweza kugundua mapema baadhi ya saratani na kuzidhibiti. Mfano wa upimaji huo ni pamoja na upimaji wa matiti na shingo yakizazi kwawanawake. Kuhusu vipimo au uchunguzi unaohitajika, pata maelezo zaidi kutoka kwa wataalamu wa afya.
Makala hii kuhusu mambo yatiba bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuSaratani kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.