Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Santo Domingo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Santo Domingo

Santo Domingo ya kihistoria (Kanisa Kuu)
Habari za kimsingi
UtawalaWilaya ya Kitaifa (Distrito Nacional)
Anwani ya kijiografiaLatitudo: 18°30′N -Longitudo: 69°59′W
Kimo14 mjuu ya UB
Eneo- 80km²
Wakazi- mji: 913,540 (2001)
- rundiko la mji: 2,500,000
Msongamano wa watuwatu 1,141 kwakm²
Simu+1809 (nchi yote)
Mahali

Santo Domingo nimji mkuu waJamhuri ya Dominikana. Ni kati yamiji ya kale kabisa yaKaribi: ilikuwa mji wa kwanza ulioanzishwa naWahispania katikaAmerika. Kunamajengo ya kwanza yahistoria ya kikoloni katika Amerika yote yaanikanisa la kwanza,chuo kikuu cha kwanza nahospitali ya kwanza.

Idadi ya wakazi ni mnamomilioni mbili.

Wakati wa udikteta waRafael Trujillo mji uliitwa "Ciudad Trijillo" (mji wa Trujillo) kati ya miaka1936 hadi1961.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Santo Domingo imekaliwa na Wahispania tangu mwaka1496 ikaundwa kama mji mwaka1498 na Bartolomeo Kolumbus (kaka yaKristoforo Kolumbus) kwenyemdomo wamto Ozama ikapewa jina "La Nueva Isabela" kwaheshima yamalkia yaHispania. Ikaharibika natufani mwaka1502 na kujengwa upya upande wa magharibi wamto.

Kanisa Kuu la Santa Maria de la Encarnación ni kanisa la kale la Amerika yote lilioanzishwa mwaka1521 na kukamilika1540. Hadi mwaka1992 lilikuwa nakaburi ambalo kwaimani ya wenyeji lilikuwa la Kristoforo Kolumbus lililohamishwa kwasherehe ya miaka 500 ya kufika kwake Amerika na kupelekwa katika jengo jipya.

Chuo Kikuu kikaanzishwa mjini mwaka1538.

Mji wa Kale uliingizwa naUNESCO katika orodha ya "urithi wa dunia".

Makala hii kuhusu maeneo yaBahari ya Karibi bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuSanto Domingo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Santo_Domingo&oldid=1328669"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp