Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Salami (chakula)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Salami jinsi zinavyotengenezwa kwa wingi kiwandani.
Aina tatu za salami za Italia.

Salami ni aina yasoseji yenyechumvi naviungo vingi isiyopikwa ikikaushwahewani au katikamoshi baridi[1].

Asili yake iko katika nchi zaUlaya,jina limetoka katikaKiitalia kutokaKilatinisalare inayomaanisha kutiachumvi.

Salami inatengenezwa kwa kuchanganyanyamanyekundu na nyama yamafuta baada ya kusaga yote mawili kwa vipande vidogo lakini ukubwa hutegemea aina yake[2].

HukoItalia zamani walitumia pia nyama yapunda nafarasi kwa soseji hiyo lakini siku hizi mara nyingi ni nyama yanguruwe. Kuna pia salami za nyama yang'ombe au nyama yandege kamabata mzinga aubuni[3].

Kimapokeo nyama iliyosagwa na kutiwa chumvi na viungo hujazwa katikautumbo lakini siku hizi salami zinatengenezwa mara nyingikiwandani ambakomirija yaplastiki hutumiwa.

Baada ya kujaza, aina nyingine hukaa tu hewani penye baridi ili zikauke na kuiva; aina nyingine huwekwa kwanza katikachumba chenyemoshi baridi ambamo zinapokealadha ya ziada halafu kukauka hewani.

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. SalamiIlihifadhiwa 28 Agosti 2016 kwenyeWayback Machine., ufafanuzi katika kamusi ya Lexico
  2. Making salame at home, tovuti ya Italia
  3. Production of salami from ostrich meat with strains of Lactobacillus sake, Lactobacillus curvatus and Micrococcus sp, makala kwenye tovuti ya science-direct

Vungo vya Nje

[hariri |hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuSalami (chakula) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Salami_(chakula)&oldid=1367543"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp