Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Romania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
România
Romania
Bendera ya RomaniaNembo ya Romania
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa:Deşteaptă-te, române!
Lokeshen ya Romania
Mji mkuuBukarest (Bucureşti)
44°25 N 26°06 E
Mji mkubwa nchiniBukarest
Lugha rasmiKiromania
SerikaliJamhuri
Klaus Iohannis
Marcel Ciolacu
Uhuru
Ilitangazwa
ilitambiluwa
9 Mei1877 (Kalenda ya Juliasi)2
13 Julai18783
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
238,391 km² (ya 82)
3
Idadi ya watu
 -2021 kadirio
 -2011 sensa
 - Msongamano wa watu
 
19,186,201[1][2] (ya 61)
19,599,506[3][4]
80.4/km² (ya 118)
FedhaLeu (RON)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD.ro
Kodi ya simu+40

-

1Lugha kamaKihungaria,Kijerumani,Kiromani,Kiukraine naKiserbia hutumiwa kieneo kwenye ngazi kadhaa

2Vita ya uhuru wa Romania.

3Mkataba wa Berlin wa 1878.


Ramani ya Romania leo.
Falme tatu chini yaMikaeli Shujaa (Mihai Viteazul) mwaka1600 hivi.
Mlima Moldoveanu, mrefu kuliko yote ya Romania.
Milima ya Rodna,Wilaya ya Maramureș.
Delta yamtoDanube.

Romania (kwaKiromania: România) ni nchi yaUlaya yakusini-mashariki.

Imepakana naHungaria,Serbia,Ukraine,Moldova naBulgaria.

Inapwani kwenyeBahari Nyeusi ambako unaishiamtoDanube.

Mji mkuu namji mkubwa zaidi niBukarest.

Historia

[hariri |hariri chanzo]

Homo sapiens aliishi katika eneo hilo walau kuanzia miaka 40,000 iliyopita.

Kabla ya kutekwa naWarumi mwanzoni mwakarne ya 2, walikuwepomakabila yaWathraki, hasaWadacha naWagete.

Chini yaDola la Roma kwa miaka 165 kulikuwa nawahamiaji wengi walioingizalugha yaKilatini.

Baadaye nchi ilitekwa na makabila mengine mbalimbali.

Katikakarne za kati kulikuwa na falme ndogotatu:Wallachia,Moldavia naTransilvania, nazo ziliendelea kuwa namadaraka fulani hata chini yaDola la Osmani hadikarne ya 18 au19.

Romania ilianzishwamwaka1859 kwa kuunganisha Moldavia na Wallachia ikapewajina hilo mwaka1866, ikajikomboa kutoka dola la Osmani mwaka1877.

Kutokana navita vikuu vya kwanza, Transilvania,Bukovina naBesarabia viliungana naUfalme wa Romania.

Katikavita vikuu vya pili, Romania iliungamkonoUjerumani dhidi yaMuungano wa Kisovieti hadi mwaka1944.

Wakomunisti waliteka nchi na baada yavita kwisha, Romania ilipoteza maeneo mbalimbali na kulazimishwa kujiunga naMapatano ya Warshawa kamajamhuri yakisoshalisti.

Baada yamapinduzi ya mwaka1989, Romania ilielekeademokrasia nauchumi wasoko huria.

Baada ya kujiunga naUmoja wa Ulaya mwaka2007, Romania imeanza kustawi na kwa sasa inaongoza pamoja naMalta zikiwa na ongezeko la 5% kwa mwaka.

Watu

[hariri |hariri chanzo]

Romania ina wakazi 19,679,306 katika eneo lakm² 238.391. Idadi yao inazidi kupungua.

Lugha rasmi ya nchi nzima niKiromania ambayo nilugha ya Kirumi kamaKiitalia,Kifaransa naKihispania, lakinilugha nyingine kadhaa zinatambuliwa nasheria, kuanziaKihungaria.

Wakazi wengi niWakristo, hasaWaorthodoksi (81%), wakifuatwa naWaprotestanti (6.2%) naWakatoliki (5.1%).

Tazama pia

[hariri |hariri chanzo]

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. "Populația rezidentă la 1 Ianuarie 2021"[The usually resident population on 1 January 2021](PDF).Insse.ro (kwa Kiromania).National Institute of Statistics. Iliwekwa mnamo30 Agosti 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Populaţia rezidentă pe sexe şi vârste, la 1 Ianuarie 2021".Insse.ro (kwa Kiromania).National Institute of Statistics. Iliwekwa mnamo30 Agosti 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Nakala iliyohifadhiwa"(PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo(PDF) mnamo 2013-12-22. Iliwekwa mnamo2013-06-22.
  4. "Nakala iliyohifadhiwa"(PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo(PDF) mnamo 2011-11-14. Iliwekwa mnamo2013-06-22.{{cite web}}:Unknown parameter|= ignored (help)


Nchi zaUmoja wa UlayaBendera ya Umoja wa Ulaya
Austria |Bulgaria |Eire |Estonia |Hispania |Hungaria |Italia |Kroatia |Kupro |Latvia |Lituanya |Luxemburg |Malta |Polandi |Slovakia |Slovenia |Romania |Ubelgiji |Ucheki |Udeni |Ufaransa |Ufini |Ugiriki |Uholanzi |Ujerumani |Ureno |Uswidi
Nchi huru
Nchi zisizokubaliwa
na umma wa kimataifa
Maeneo yanayojitawala
chini ya nchi nyingine
1 nchi yaAsia ya Magharibi kijiografia ambayo huhesabiwa kuwa sehemu yaUlaya kiutamaduni2nchi ya kimabara
Makala hii kuhusu maeneo yaUlaya bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuRomania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Romania&oldid=1290700"
Jamii:
Jamii zilizofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2026 Movatter.jp