Robert Mugabe |
---|
Robert Mugabe 2009 |
|
Tarehe ya kuzaliwa | 21 Februari 1924 |
Tarehe ya kifo | 6 Septemba 2019 |
Chama | ZANU |
Kazi | Rais |
Robert Gabriel Mugabe (21 Februari1924 -6 Septemba2019) alikuwakiongozi mkuu waZimbabwe tangu1980 hadi2017. Alikuwamwenyekiti wachama tawala chaZANU.
Mwaka 1980 alikuwawaziri mkuu na mwaka1987Rais wa Zimbabwe. Kabla ya wakati ule aliongoza upinzani wa ZANU dhidi yaserikali yawaloweziWaingereza nchini waliofuatasiasa yaubaguzi wa rangi.
Mugabe alirudia kushinda katikauchaguzi mara kadhaa. Tangu mwaka 2000 chaguzi hizo zilitiwa shaka kutokana na matishio na matumizi ya mabavu dhidi ya wapinzani.Utawala wa Mugabe umeitwa wakidikteta tangu mwaka2002. Kutokana na mashtaka dhidi ya serikali ya Mugabe ya kudharauhaki za binadamu, nchi ya Zimbabwe ilisimamishwa ndani yaJumuiya ya Madola. Mugabe pamoja namawaziri wake na viongozi wa chama chake hawakuruhusiwa kusafiri kwenda nchi zaUmoja wa Ulaya naMarekani.
Mwanzoni mwa utawala wake Mugabe alisifiwa kujengauchumi na sera yaelimu nchini. Zimbabwe ilikuwa nchi iliyouzachakula kwa wingi nje. Tangu mwanzo wamilenia mpya pamoja na mashtaka ya udikteta hali ya uchumi ilirudi nyuma. Takribanraiamilionimbili wa Zimbabwe wameondoka nchini wakakaa kamawakimbiziAfrika Kusini.
Tuhuma za mauaji na ukandamizaji
Nchi hiyo ilikuwa tayari imegawanyika kikabila hata katika uchaguzi wa kwanza wa 1980, Mashona wote walimchagua Mugabe naWandebele nawabunge kutoka chama cha ZANU. Wakati Wandebele walichagua viongozi kutoka chama chaZAPU kilichoongozwa naJoshua Nkomo.
Baada tu ya kushikamadaraka, Mugabe aliamua kukandamiza upinzani dhidi yake aliyoona kati ya wanachama wa ZAPU na wanajeshi wake wa ZIPRA waliowahi kurudi. Alishinda majaribio ya uasi wa askari waZIPRA 1980 kwa msaada wa vikosi vya Rhodesian Defence Force. 1981 Mugabe aliunda kikosi kipya cha "Brigedi ya Tano" kilichofanywa na wanamgambo waZANLA wa awali (jeshi la chama chake ZANU) na kufundishwa na washauri kutoka Korea Kaskazini. Brigedi hii ilitumwa katika maeneo ya Wandebele katika kusini ya Zimbabwe (mazingira yaBulawayo) kutafuta askari wa ZIPRA mafichoni; katika mauaji yaGukurahundi yaliyoendelea hadi 1984 ni Wazimbabwe 20,000 wanakadiriwa waliuawa.
Ingawamauaji hayo hayakufikia kiwango cha yale yaRwanda naBurundi, waliuawawanawake,wanaume,watoto na hata vichanga vilivyokuwa matumboni.
Kuanzia enzi hizo rais Mugabe amejaribu kushinda kila uchaguzi nchini huko kwa kutumia nguvu za kikabila na mabavu.
 | Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuRobert Mugabe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari. |