Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Rakim

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rakim
Rakim akitumbuiza mnamo 2008
Taarifa za awali
Jina la kuzaliwaWilliam Michael Griffin Jr.
Pia anajulikana kamaThe God MC, Kid Wizard, The R, The 18th Letter, Rakim Allah
Amezaliwa28 Januari1968 (1968-01-28) (umri 57)
Wyandanch, New York, U.S.
Kazi yakeRapa, mtunzi wa nyimbo, mtayarishaji wa rekodi
Eric B. & Rakim

William Michael Griffin Jr. (alizaliwa28 Januari,1968), anajulikana zaidi kwa jina lake la kisaniiRakim(/rɑːˈkɪm/), ni rapa kutoka nchiniMarekani. Ni msanii mwenza wa enzi zakizazi cha dhahabu cha hip hop—Eric B. & Rakim, ambao walitoa albamu nne: Paid in Full (1987), Follow the Leader (1988), Let the Rhythm Hit 'Em (1990), na Don't Sweat the Technique (1992). Pia ametoa albamu nne kama msanii wa kujitegemea: The 18th Letter (1997), The Master (1999), The Seventh Seal (2009), na G.O.D.'s Network: Reb7rth (2024).

Rakim huhesabiwa kama mwanampinduzi hip hop kwa kusogeza mbele mbinu za MC kwa kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa hapo awali. Alisaidia kuanzisha matumizi ya mizani ya ndani (internal rhymes) na mizani yenye silabi nyingi (multisyllabic rhymes). Rakim alikuwa miongoni mwa wasanii wa kwanza kuonyesha uwezo wa kuandika mashairi yaliyochongwa kwa ustadi. Mashairi yaliyojaa maneno ya busara na tamathali za semi, badala ya kutumia mitindo ya uchanaji wa kujirudiarudia na mifumo rahisi ya mizani iliyotawala kabla yake.[1] Pia anapewa sifa kwa kuleta mabadiliko kutoka kwa mitindo rahisi ya awali ya hip hop hadi mitiririko tata zaidi.

RapaKool Moe Dee alieleza kuwa kabla ya Rakim, neno flow (kughani) halikutumika sana – "Rakim kimsingi ndiye mvumbuzi wa flow. Hatukuwa tunatumia neno hilo kabla yake. Ilikuwa inaitwa uchanaji wa mashairi (rhyming), au mpangilio wa midundo (cadence), lakini haikuitwa flow. Rakim alibuni flow!"[2]

Albamu Paid in Full ilitajwa kuwa albamu bora zaidi ya hip hop ya wakati wote na MTV mnamo 2006, huku Rakim mwenyewe akishikilia nafasi ya nne kwenye orodha ya MTV ya MC wakubwa wa muda wote.[3] Steve Huey wa AllMusic alisema kuwa "Rakim anaheshimiwa karibu na kila mtu kama mmoja wa MC bora zaidi – labda bora zaidi – wa wakati wote ndani ya jamii ya hip hop." Wahariri wa About.com walimuweka nafasi ya pili kwenye orodha yao ya Top 50 MCs of Our Time (1987–2007). Mnamo 2012, The Source ilimuweka namba moja kwenye orodha yao ya Top 50 Lyricists of All Time.[4]

Diskografia

[hariri |hariri chanzo]

Albamu

[hariri |hariri chanzo]

Albamu za kujitegemea

With Eric B. & Rakim

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]
  1. "Rakim Songs, Albums, Reviews, Bio & More | All..."AllMusic (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo2025-02-09.
  2. "Rakim",Wikipedia (kwa Kiingereza), 2024-12-28, iliwekwa mnamo2025-02-09
  3. "MTV.com: The Greatest Hip-Hop Albums Of All Time".web.archive.org. 2013-07-19. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2013-07-19. Iliwekwa mnamo2025-02-09.
  4. "MTV.com: The Greatest MCs Of All Time".web.archive.org. 2012-04-18. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutokachanzo mnamo 2010-04-02. Iliwekwa mnamo2025-02-09.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Rakim&oldid=1398466"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp