Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Radi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa maana tofauti ya neno hili kama elementi ya kikemia angaliaradi (elementi)

Radi nchini Marekani

Radi (pia:ngurumo ya umeme) ni mwangaza namiale yamwanga mithili yashoti zaumeme inayotokea wakati wa ngurumo wamvua ya radi.Neno radi linaweza kutaja piasauti yenyewe na mwanga katikati yamawingu unaweza kuitwa "umeme".

Matumizi ya neno "umeme" kwa ajili yateknolojia ya "stimu" (jinsielectricity inavyoitwa nchiniKenya) navifaa vya umeme yamesababisha kukaza tofauti kati ya umeme kwa jumla na kutokea kwake kwa ghafla wakati wamvua kali kama mwangaza mkali. Hata hivyo maana asili ya "umeme" ni ule mwangaza.

Asili yake nivolteji inayojijenga kati ya mawingu angani yenyechaji tofauti au pia kati ya mawingu naardhi. Volteji hiyo ikiongezeka mno husababishamkondo wa umemehewani unaoonekana kama mwangaza mkali. Mkondo unatoa piajoto kali na joto hilo husababisha kupanuka kwa hewa ghafla. Upanuzi huo unaleta sauti inayosikika kama ngurumo kama ni mbali, lakini inaweza kusikika pia sawa na mshtuko wamlipuko kama ni karibu.

Kama mwendo wa radi ni kutoka mawinguni kwenda ardhi unaweza kuleta hasara kwawatu auvitu. Takriban watu 2,000 hupigwa na radi kilamwaka na mara nyingi wanakufa. Radi huwashamoto kwenyenyumba aupori.

Radi inayolenga ardhi huelekea kuingia sehemu ya juu mahali inapopiga. Hapo kuna mitambo yakikingaradi[1]: nichuma zilizopo juu yadari ya nyumba na kuendelea hadi ndani ya ardhi kando ya nyumba. Kama radi inapiga nyumba itachukua njia ya haraka ya kufika ardhini kwa hiyo itapita kwenye vyuma bila kuharibu nyumba yenyewe.

Tofauti ya madhara yaliyopo kati ya radi na ngurumo hutegemeana na kiwango cha athari zinazojitokeza. Kwa kuwa ule wa radi ni umeme mkubwa sana, hivyo basi madhara yake ni makubwa sana kulinganisha na sauti kubwa na ya kuogofya inayotokea muda mfupi tu baada ya radi kutokea.

Tanbihi

[hariri |hariri chanzo]
  1. An earth wire is literally a wire that goes down into the earth - also known as an “earth ground.” It's meant to be the electrical path that unwanted electricity (such as lightning or a short-circuit) finds easiest to take.

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo yasayansi bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuRadi kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Radi&oldid=1370447"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp