Mwimbaji-mtunzi-wa-nyimbo,rapa, mwanamuziki, mtayarishaji wa rekodi, mtayarishaji mtendaji, mtendaji wa rekodi, mpiga vyombo vingi-vingi, mwongozaji wa muziki wa video
Robert Sylvester Kelly (amezaliwa tar.8 Januari1967) ni mwimbaji wa muziki waR&B nasoul-mtunzi wa nyimbo,rapa, na mtayarishaji wa rekodi kutoka nchiniMarekani. Anafahamika zaidi kwajina la kisanii kamaR. Kelly. Alianza kuingia katika kazi ya muziki kwa mara kwanza kunako mwaka wa 1992 akiwa na kundi laPublic Announcement, halafu baadaye Kelly akaenda kuwa kama msanii wa kujitegemea mnamo 1993 na kuweza kupata mafanikio makubwa kabisa kwa kazi za kujitegemea baada ya kutoa albamu yake ya12 Play.
Kelly pia ametayarisha na kuimba katika nyimbo nyingine kibao za wasanii wengine wa R&B na hip-hop. Mnamo mwaka wa 1994, Kelly ametayarisha na kutunga albamu ya kwanza ya mwimbaji wa R&BAaliyah na mwaka wa 1995, Kelly ameshiriki-kutayarisha na kutunga wimbo wa "You Are Not Alone" kwa ajili yaMichael Jackson, ambao uliingizwa kwenye albamu ya Jackson,HIStory.
Katika maisha yake binafsi, Kelly amekuwa na kashfa kadhaa za ngono. Taarifa zilielezwa kwamba amemwoa kabinti kadogo Aaliyah, ambaye yeye ndiye alikuwa mtunzi wake wa nyimbo. Kelly na Aaliyah wakasitisha ndoa yao. Baada ya kutolewa video ya mtu moja aliyedaiwa kuwa yeye kufanya mapenzi na msichana mdogo, Kelly akashtakiwa katika kesi kadhaa za ngono za watoto mnamo 2002.[1] Baada ya makawio kadhaa, kesi yake ikapelekwa kizimbani mnamo 2008, na baraza la wazee wa mahakama likamwona Kelly hana kosa katika mshtaka yote 14.[2]
Januari 2019 kipindi cha televisheni chaLifetime kilitoa filamu fupi iitwayoSurviving R. Kelly iliyoonyesha wanawake wanaomshutumi kwaunyanyasaji wa kingono. Kutokana na tuhuma hizo, kampuni yaRCA Records ilufuta mkataba wake na Kelly.[3] Februari 22, 2019, Kelly alifunguliwa mashtaka mengine 10.[4] Julai 11, 2019, Kelly alikamatwa kwa mashataka kadhaa ya ngono.[5][6] Hadi Julai 12, 2019, Kelly anakabiliana na mashtaka 18 ikiwa ni pamoja na kufanya mapenzi na watoto wadogo, kuteka nyara na kazi ya kulazimishwa.[7]
1998: Mwimbaji na Mtunzi Bora wa Pop wa Mwaka (kwa ajili ya “I Believe I can Fly”, “I Can’t Sleep Baby (If I)”, na “I Don’t Want To” (imerekodiwa naToni Braxton)
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Marekani bado nimbegu. Je, unajua kitu kuhusuR. Kelly kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.