Quito(tamka: "kito" - Kihisp. "San Francisco de Quito") nimji mkuu waEkuador. Mwaka2005 ilikuwa na wakazi 1,865,541. Quito ni mji mkubwa wa pili nchini baada yaGuayaquil.
Mji uko 20 km kusini ya mstari waikweta katika bonde la milima yaAndes kwenye kimo cha 2850m juu yaUB.
Kuna kiwanja cha ndega na chuo kikuu pamoja na viwanda.
Quito ilikuwa kati ya miji muhimu ya Dola la Inka kabla ya kufika kwa Wahispania. Wakati wa uvamizi wa Wahispania jenerali Rumiñahui wa jeshi la Inka alichoma mji na kuiharibu kabisa kabla ya Wahispania hawakuiteka.
Mwaka 1809 wakati wa ghasia katika sehemu mbalimbali zaAmerika Kusini dhidi ya serikali ya mfalme mpya wa HispaniaJoseph Bonaparte (mdogo wakeNapoleon Bonaparte) kamati ya raia katika Quito ilitangaza uhuru wa eneo lake kutoka Hispania. Utawala wa Hispania ulirudishwa kwa mabavu hadi 1822 wakati Hispania ilishindwa na mapinduzi yaSimon Bolivar na kuundwa kwa jamhuri yaGran Colombia. Baada ya mwisho wa jamhuri hii sehemu zake ziliachana Quito ikawa mji mkuu wa nchi mpya ya Ekuador.
Makala hii kuhusu maeneo yaAmerika Kusini bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuQuito kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.