Punyeto (kwaKiingereza:masturbation]) ni tendo lolote la kujitafutiaashiki binafsi hasa kwa kuchocheaviungo vya uzazi. Wanaochukua hatua hiyo ili wajipatie kionjo cha kuridhisha kinachofanana na kile chatendo la ndoa kwa kawaida wanasukumwa namsisimko uliowapata, pamoja nahaya ya kujitafutia mwenzi nahofu ya kuambukizwamaradhi ya zinaa.
Kufanya hivyo ni kupotosha maana yajinsia kwabinadamu, ambayo ni kufanya wawili wawe kitu kimoja kwa nguvu yaupendo ambao uanzerohoni na kukamilika katika muungano wa miili yao.
Upendo maana yake ni kujitoa kwa muungano na mpenzi unaoletatunda lake katikamtoto, ambaye ni kwa pamoja wababa na wamama, akiwaunganisha upya ndani mwake.
Katika tendo la kujichua hakuna lolote kati ya hayo: hakuna upendo wala kujitoa kwa wengine, hakuna muungano walauzazi, isipokuwa kujitafutia iwezekanavyofuraha ya kimwili (ashiki) iliyokusudiwa naMungu kuwa sehemu ya furaha nzima ya muungano wa ndoa.
Katika tendo hilo laubinafsi mtu yuko peke yake na kubaki peke yake: halengi chochote nje yamwili wake, hivyo anazidi kuzama ndani mwake badala ya kustawi kwa kujiwekea malengo mema (k.mf.ndoa,haki,huduma kwa wenye shida,utume n.k.). Matokeo yake ni kupotezanguvu za mwili na hasa kuvuruga msimamo wanafsi kwa kujisikia mnyonge, mwenye kosa na mtumwa wa tendo ambalo analikinai mara tu baada ya kulitenda. Hatimaye anaweza kupata matatizo katika tendo la ndoa.
Kwa msingi huoKanisa Katoliki linahesabu punyeto kuwadhambi kubwa, tena upande mmoja ni kubwa kulikouasherati (kuzini kati ya msichana na mvulana), kwa sababu linakwenda kinyume chamaumbile na kuandaa njia kwa dhambi nyingine (k.mf.ushoga)[2].
Hata hivyoelimunafsia inatueleza pia urahisi kwa mtu asiyekomaa kimapendo kufuata njia hiyo danganyifu, tena ngumu kuachwa baada ya kuzoeleka mpaka ukawauraibu wa punyeto[3].
Ndiyo sababuKanisa linamhimizapadri kupokea kwahuruma wenye tatizo hilo na kuwasaidia mashauri ya kibinadamu pia kuhusuafya ya mwili na ya nafsi. Kwa mfano: kunyoshaviungo kwakazi za mikono au kwamichezo, kulalia pagumu tena si kifudifudi, kukwepa vinywaji vinavyochocheaneva (kahawa,chai n.k.), kushirikiana zaidi na watu, kusaidia wenye shida. Upande wa roho awashauri kufuata vizuridini. Awatumainishe wanaweza kushinda, kwa hiyo wasikate tamaa wala wasiogope mno.
Kutumia punyeto kunaweza kuleta matatizo kwa njia ya uzazi na kushindwa kuenezambegu za uzazi wakati wa kujamiana[4]</ref>.
Hata hivyo kuna madaktari wanaohimiza punyeto na kusema ni njia ya kuonyesha pendo binafsi na ni kitendo cha kawaida kabisa kisicho na madhara yoyote katika maumbile ya uzazi. Tena wanasema mtu anapopiga punyetokemikali yaendofini hutolewa ambayo inafanana nadawa za kulevya na hivyo husaidia kwa muda mfupi kupunguzamaumivu namsongo wa mawazo.
Watu wengine wanatetea punyeto na kuipendekeza kama njia ya kuzuia uenezi waukimwi.
Bila shaka wanaofanyabiashara ya vifaa vya kujichulia naponografia wako mstari wa mbele kuhimiza punyeto tanguutotoni.
↑Katekisimu ya Kanisa Katoliki, "Article 6: The Sixth Commandment", cfr. www.vatican.va. p. 2352, inafundisha: "By masturbation is to be understood the deliberate stimulation of the genital organs in order to derive sexual pleasure. "Both the Magisterium of the Church, in the course of a constant tradition, and the moral sense of the faithful have been in no doubt and have firmly maintained that masturbation is an intrinsically and gravely disordered action." "The deliberate use of the sexual faculty, for whatever reason, outside of marriage is essentially contrary to its purpose." For here sexual pleasure is sought outside of "the sexual relationship which is demanded by the moral order and in which the total meaning of mutual self-giving and human procreation in the context of true love is achieved." To form an equitable judgment about the subjects' moral responsibility and to guide pastoral action, one must take into account the affective immaturity, force of acquired habit, conditions of anxiety or other psychological or social factors that lessen, if not even reduce to a minimum, moral culpability."
↑According to DSM-5-TR, "Delayed ejaculation is associated with highly frequent masturbation, use of masturbation techniques not easily duplicated by a partner, and marked disparities between sexual fantasies during masturbation and the reality of sex with a partner." Cfr. "American Psychiatric Association 2022 ch. 16":American Psychiatric Association (2022). "Sexual Dysfunctions".Diagnostic and Statistical Manual of Mental Disorders, Fifth Edition, Text Revision (DSM-5-TR(tm)). G - Reference, Information and Interdisciplinary Subjects Series. American Psychiatric Association Publishing. uk. 479.ISBN978-0-89042-576-3.