Spishi kadhaa wana tofauti kubwa kati yadume najike; dume wa spishi hizo wanaweza kuwa na uzito mara mbili kuliko jike na pia kuonyesharangi tofauti kama nyani waPapio hamadryas.
Primata wengi hukaliamiti naviungo vyao vinalingana namaisha yao. Kwa spishi nyingi miguu ni mikubwa na yenyenguvu zaidi kuliko mikono, isipokuwaGiboni waAsia Kusini-Mashariki na sokwe wakubwa wasio binadamu.
Katika spishi zinazotembea mtini kwa kuning’inia kwa mikonokidole gumba kimefifia.
Mkia ni muhimu kwa primata wengi wanaoishi mtini lakini spishi nyingine wana mkia mdogo au hawana. Nyani kadhaa waAmerika wana mkia wa kushikilia usio na nywele upande wa chini wenyeneva muhimu.
Mwili wa primata wengi umefunikwa nanywele zenye rangi baina yanyeupe,kijivu,kahawia hadinyeusi. Viganja kwa kawaida havina nywele. Spishi kadhaa hazina nyweleusoni. Binadamu ni spishi yenye nywele chache.
Inaaminiwa kuwa primata kiasili waliishi mtini na hadi leo wengine wana maisha yao mtini pekee ambao hawatembei ardhini. Wengine wanaishi chini na juu pia. Wanaotembea kwenye uso wa ardhi pekee ni wachache pamoja na binadamu.
Spishi nyingine zinaogopamaji lakini kuna pia aina zinazopenda maji zinajua hata kuogelea. Spishi kadhaa zimezoeamazingira ya binadamu zinazoishi kwenyevijiji namiji kama makaka waUhindi.
Kimsingi strepsirhini (wenye pua bichi) wanafanya shughuli zao wakati wausiku na kulalamchana lakini haplorhini (wenye pua kavu) wanafanya shughuli zao machana na kulala usiku. Wale wanaofanya shughuli zao usiku kwa jumla ni wadogo zaidi na wana uwezo mzuri zaidi wa kunusu.
Sawa na mamalia wengine wale wanaokula hasamajani wanapumzika muda mrefu zaidi wakihitaji muda mrefu kumeng'enyachakula chao.