Ardhi ya Polandi ni tupu tu kufikia kiasi chaBahari ya Baltiki katika upande wa kaskazini mwaMilima ya Carpathi kusini mwa nchi. Ndani ya eneo hilo lililo tupu, ardhi inatofautiana kutoka mashariki na magharibi.
Pwani ya Kipolandi ya Bahari ya Baltiki ni murua zaidi, lakini inabandari asilia katikamkoa waTrójmiasto:Gdańsk,Gdynia naSzczecin huko mashariki-magharibi ya mbali. Pwani hiyo inaupepo mzuri na maeneo kadhaa ya pwani za maziwa. Pwani za maziwa na fukwe za zamani ambazo zimekatwa kutokabaharini. Sehemu hizi pia huitwarasi.Rasi ya Szczecin ipo upande wa mashariki mwa mpaka wa nchi yaUjerumani.Rasi ya Vistula ipo upande wa mashariki mwa mpaka wa mji waKaliningrad, ambao ni katika mkoa waUrusi.
Mto mrefu zaidi nchini Polandi niVistula, unaoangukia ndani ya Rasi ya Vistula na pia unakwenda moja kwa moja hadi katika Bahari ya Baltiki. Nikm 1064 kutokachanzo hadimdomo.
Kanda ya kaskazini-mashariki ni miti tu imejaa, inakosa watu wachache narasilimali za kilimo na viwanda. Kanda ya kijografia inawilaya nne za vilima vya moraine na maziwa yaliyotengenezwa na moraine. Haya yalianzishwa baada yaPleistoceneZama za Barafu. Ziwa Masurian ni miongoni mwa maziwa manne ya wilaya yaliyochukua eneo kubwa la kaskazini-mashariki mwa Polandi.
Polandi ina maziwa kibao. KwaUlaya nzima,Finland peke yake ina maziwa mengi zaidi. Maziwa makubwa ni "Śniardwy" na "Mamry". Kwa kuongeza katika wilaya ya ziwa katika kaskazini, kuna idadi kubwa pia ya mlima maziwa katikamilima ya Tatra.
Ukiendelea na safari kusini ni mlima ya kanda ya Kipolandi. Milima hiyo ni pamoja naSudetes naMilima ya Carpathi. Sehemu ndefu yaCarpathia ni milima ya Tatra ambayo imekwenda hadi kusini mwa mpaka wa nchi ya Polandi.
Mlima mrefu zaidi nchini Polandi unaitwa "Rysy" wenyem 2,503 (ft 8,210), upo Tatras.
Katika miaka ya1569–1795 Polandi iliunganishwa naLituanya katikashirikisho la kifalme. Mfalme wa Polandi alikuwa pia mtawala wa Lithuania, na tangumapatano ya Lublin nchi hizo mbili zilikuwa nabunge la pamoja, lakini kila sehemu iliendelea nasheria zake najeshi la pekee. Bunge la pamoja lililokuwa hasa mkutano wamakabaila wote lilikuwa namamlaka ya kumchagua mfalme likapata ushawishi mkubwa.
Wagombea wa ufalme waliachana na mamlaka za kifalme wakijaribu kupatakura nyingi za wabunge na hivyo nguvu ya dola ilififia.
Mwaka1764 nchi ilianza kurudi nyuma na zile za jirani, yaani Urusi, Austria na Prussia, ziligawana kwa awamu tatu (1772,1793,1795) eneo lake lote. Yaani kuanzia mwaka1772 majirani hayo matatu ya Polandi yalivamia shirikisho na kugawana maeneo yake. Kufikia mwaka1795 maeneo yote yalikwisha kugawiwa kati ya majirani hao.
Wapolandi walijaribu mara kadhaa kujikomboa, lakini walipatauhuru kwa muda tu (1807-1815 na1918-1939).
Makala hii kuhusu maeneo yaPolandi bado nimbegu. Je unajua kitu kuhusuPolandi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.