Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Plutoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Plutoni (plutonium)
kipande duara cha plutoni
kipande duara cha plutoni
Jina la ElementiPlutoni (plutonium)
AlamaPu
Namba atomia94
Mfululizo safuMetali
Uzani atomia244
Valensi2, 8, 18, 32, 24, 8, 2
Densiti19.816  g·cm³
Kiwango cha kuyeyuka912.5 K (639.4°C) 912,5 K ( °C)
Kiwango cha kuchemka3505 K (3228 °C) K ​(3228 °C,
Asilimia zaganda la dunia2 · 10-16 %
Hali maadamango
Mengineyonururifu sana

Plutoni nielementi katikamfumo radidia yenyealamaPu.Namba atomia ni94 nauzani atomia ni 244.Jina limechaguliwa kutokana nasayari kibetePluto.

Plutoni nimetalinururifu. Kiasili inatokea katika viwango vidogo sana penye madini yaurani kutokana nambunguo nyuklia wa elementi hiyo ambao unaweza kuzalisha elementi nyingine. Vile viwango vidogo haviwezi kukaa mud mrefu kutokana na nusumaisha fupi ya plutoni inayozalishwa humo. Sehemu kubwa iliyopo leo hii imezalishwa katika matanuri ya nyuklia kutokana naurani.

Matumizi yake ni katika matanuri ya nyuklia na katikasilaha za nyuklia. Matumizi yake ya kijeshi yalitangulia matumizi mengine:bomu lililobomoamji waNagasaki nchiniJapan katika Agosti1945 na kusababisha vifo 60,000 lilitengenezwa kwa plutoni.

Umuhimu wa kiuchumi

[hariri |hariri chanzo]

Inatokea mara kwa mara kwa kuchoma urani katikatanuri nyuklia. Hivyo inasafishwa na kurudishwa kamafueli katika aina tofauti za matanuri ya nyuklia.

Matatizo yake ni kwambaunururifu wake ni mkali na hivyo kuna hatari ya kuishughulikia katika matumizi. Viwango vidogo sana vya plutoni vinaweza kusababishakansa kama elementi hii inaingiamwilini kamavumbi au katikachakula. Baada ya kuzalishwa Plutoni inaendelea kuwa nururifu kwa muda mrefu na hivyo takataka ya kinyuklia yenye plutoni inahitaji kutunzwa mbali na watu kwa vipindi wa miaka elfu hata makumi elfu kadhaa.

Matumizi ya pekee ya plutoni ni katikabeteri kwa ajili yavyombo vya angani hasa vile vinavyokwenda mbali najua na hivyo haviwezi kutumianishati ya jua.

Makala hii kuhusu mambo yakemia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuPlutoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu mambo yafizikia bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuPlutoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Plutoni&oldid=1105140"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp