Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Plataia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mabaki ya ukuta wa Plataia ya Kale

Plataia auPlataea (kwaKigirikiΠλάταια) ulikuwamji waUgiriki ya Kale, uliokoUgirikikusini, takribankilomita 60 upande wamagharibi mwaAthens, kusini mwaThebes.

Plataia ilikuwa mjirafiki wa Athens na katikavita dhidi yaWaajemijeshi la Plataia lilipigana pamoja na Waathens kama kwenyemapigano ya Marathon mnamomwaka490 KK.Mapigano ya Plataia yaliyotokea mnamo479 KK karibu na mji yaliyetaushindi wa mwisho wa Wagiriki dhidi ya Uajemi.

Plataia iliharibiwa katikaVita ya Peloponnesi na Thebes naSparta mnamo427 KK ikajengwa upya mnamo386 KK na kubomolewa tena373 KK.

Mji wa kisasa wa Plataies umejengwa karibu namagofu yake.

Kilima cha mazishi cha Waplataia waliouawa kwenyeMapigano ya Marathoni

Marejeo

[hariri |hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri |hariri chanzo]
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Plataia&oldid=1135907"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp