Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Pesa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pesa yaEuro

Pesa ni chombo cha kubadilishanabidhaa nahuduma kati ya watu. Pesa yenyewe haina faida, haitoshelezi mahitaji yabinadamu ila imekubalika katikajamii kama njia ya kujipatia mahitaji mengine.

Kuna maneno mengine yaKiswahili kwa pesa kama vilehela,fedha ausarafu.

Mfumo wa sarafu unamaanishautaratibu wa kutoa na kusimamia pesa katikauchumi wa kisasa.

Historia ya pesa

Sarafu ya mwaka640 KK kutokaLydia

Kiasili watu walibadilishana vitu kwa mfanong'ombe mmoja kwambuzi kadhaa au mazao kwasamaki n.k.

Baadaye imeonekana ya kwamba itasaidia zaidi kamakiwango fulani inapatikana kwa vitu vyote.

Metali zilizokuwa haba zilitumiwa kamakipimo hiki, kwa mfanodhahabu,fedha aushaba. Vilipimwa kufuatana nauzito.

Hatua iliyofuata ilikuwa kutumia vipande vya metali hizi vilivyogongwa mihuri halafu hapakuwa na lazima ya kuvipima kimoja-kimoja. InavyojulikanaWachina walikuwa watu wa kwanza waliochukua hatua hii katikamilenia ya 2 KK. Hii ilikuwa mwanzo wasarafu.

Pesa hutolewa naserikali ya nchi au nataasisi kamabenki kuu inayofanya kazi hii kwa niaba ya serikali. Mwanzoni sarafu ilikuwa sawa nakiasi fulani cha dhahabu au fedha.

Hatua nyingine ilikuwa kutolewa kwa pesa yakaratasi aubenknoti zilizoahidi kumpatia mtu yeyote kiasi kilichoandikwa kwa dhahabu au fedha yenyewe. Kwa muda mrefu benki kuu zilikuwa nahazina ya dhahabu iliyolingana na kiasi cha benknoti zilizochapishwa.

Tangu mwisho wakarne ya 20 nchi kadhaa zilianza kutoa benknoti zaplastiki kwa sababu zinadumu kushinda noti zakaratasi, tena ni vigumu zaidi kwa wajanja kutengenezapesa bandia.

Katika karne ya 20 nchi zote zilifanya hatua ya kuacha makadirio ya dhahabu kwa sababuthamani ya bidhaa katika jamii ilipita kiasi cha dhahabu iliyopatikana. Siku hizi jumla ya pesa inayotolewa inatakiwa kulingana na thamani yarasilmali ya taifa fulani.

Pale ambako serikali inachapisha benknoti kushinda kiwango hicho, thamani ya pesa inashuka namfumko wa bei unatokea.

Pesa 1 ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani (hadi 1904) - nyuma; maandishi yasema: "Deutsch-Ostafrikanische Gesellschaft 1892"

Asili ya neno "Pesa" katika sarufi ya Kihindi

Asili ya neno "pesa" katika lugha yaKiswahili ni sarufi ndogo ya Kihindi iliyokuwakitengo charupia. Rupia 1 ilikuwa na "paisa" 64 ikawa sarufi ya kawaida katikaAfrika ya Mashariki kabla ya kipindi chaukoloni. Neno la kiasili "paisa" likanyoshwa kuwa "pesa".

"Pesa" ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani

Wajerumani walipoanzisha koloni laAfrika ya Mashariki ya Kijerumani waliendelea kutoa sarafu kwa jina la rupia na pesa hadi 1904. Pesa 64 zilifanyarupie 1. Mwaka1904 walibadilishamuundo na sarafu ya pesa ilipotea, badala yakeheller ilianzishwa. Lakini neno lilibaki katikalugha.

Sarafi za pesa zilitolewa naKampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki. Zilikuwa na maandishi yaKiarabu upande mmoja na maandishi yaKijerumani nyuma yake. Upande wa Kiarabu ulionyeshamwaka wa kutolewa kama tarehebaada ya hijra na upande wa Kijerumani ulionyesha mwakaBK. Maandishi yalikuwa jina la kampuni tu kwa Kiarabu na Kijerumani; upande wa Kijerumani ulikuwa natai mwenyetaji kama nembo laMilki ya Ujerumani.

Pesa za dunia

Pesa za dunia zinazotumiwa zaidi kimataifa
Pesa za nchi mbalimbali zinazotumiwa katika biashara ya kimataifa na asilimia yao katika biashara ya pesa
utengezaji wa pesa mjini Perm
PesaKifupi
(alama)
% ya biashara
(Aprili 2013)
MarekaniDollar ya MarekaniUSD ($)87.0%
EuroEUR (€)33.4%
JapaniYen ya JapaniJPY (¥)23.0%
Ufalme wa MuunganoPauni ya UingerezaGBP (£)11.8%
AustraliaDollar ya AustraliaAUD ($)8.6%
UswisiFrank ya UswisiCHF (Fr)5.2%
KanadaDollar ya KanadaCAD ($)4.6%
MexikoPeso ya MexikoMXN ($)2.5%
Jamhuri ya Watu wa ChinaRenminbi (Yuan) ya ChinaCNY (¥)2.2%
New ZealandDollar ya New ZealandNZD ($)2.0%
UswidiKrona ya UswidiSEK (kr)1.8%
UrusiRubel ya UrusiRUB (₽)1.6%
Hong KongDollar ya Hong KongHKD ($)1.4%
Dollar ya SingapurSGD ($)1.4%
UturukiLira ya UturukiTRY (₺)1.3%
Pesa za nchi nyingine12.2%
Jumla (jumla imekadiriwa kuwa 200% kwa sababu biashara ya pesa za kimataifa inahusu aina mbili tofauti)200%

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu mambo yauchumi bado nimbegu.
Je, unajua kitu kuhusuPesa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Pesa&oldid=1397745"
Jamii:
Jamii iliofichwa:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp