Movatterモバイル変換


[0]ホーム

URL:


Nenda kwa yaliyomo
WikipediaKamusi elezo ya maandishi huru
Tafuta

Uajemi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutokaPersia)
جمهوری اسلامی ايران
Jomhūrī-ye Eslāmī-ye Īrān

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (Uajemi)
Bendera ya UajemiNembo ya Uajemi
BenderaNembo
Kaulimbiu ya taifa:Kiajemi:Esteqlāl, āzādī, jomhūrī-ye eslāmī
("Uhuru, Huria, Jamhuri ya Kiislamu")
Wimbo wa taifa:Sorūd-e Mellī-e Īrān
Lokeshen ya Uajemi
Mji mkuuTehran
35°40′ N 44°26′ E
Mji mkubwa nchiniTehran
Lugha rasmiKiajemi (Farsi)
SerikaliJamhuri ya Kiislamu
Ali Khamenei (سید علی خامنه‌ای)
Ebrahim Raisi (سیدابراهیم رئیسی)
Mapinduzi
imetangazwa

11 Februari1979
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
1,648,195 km² (ya 18)
0.7%
Idadi ya watu
 -2013 kadirio
 -1996 sensa
 - Msongamano wa watu
 
78,192,200[2] (ya 18)
60,055,488[1]
48/km² (ya 162)
FedhaRial (ريال) (IRR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+3.30)
not observed (UTC+3.30)
Intaneti TLD.ir
Kodi ya simu+98

-



Uajemi (kutokana naKiarabuالعجم- al-'ajam) ni nchi yaAsia ya Magharibi. Kimataifa inajulikana zaidi kwa jinaIran (ايران).

Jina rasmi ya nchi niJamhuri ya Kiislamu ya Iran au Uajemi. Uajemi imejulikana tangu kale kama nchi iliyochangia mengi katikahistoria yabinadamu.

Imepakana naAfghanistan,Armenia,Azerbaijan,Iraq,Pakistan,Uturuki naTurkmenistan.

Upande wakusini kunamwambao waGhuba ya Uajemi (Bahari Hindi) na upande wakaskazini ni mwambao waBahari ya Kaspi.

Tehran nimji mkuu, pia mji mkubwa nchini.

Historia

Tangu mwaka500KK makabila madogo ya nchi yaliunganishwa, na hii ilikuwa mwanzo wamilki ya Uajemi.MfalmeKoreshi II aliunganisha Uajemi wote chini yamamlaka yake akavamia sehemu zaUturuki wa leo naBabeli na kuunganisha nchi hizo.

Waandamizi wake walipanua milki hadiMisri,Uhindi naUgiriki.

Milki hiyo ilikwisha baada ya kushindwa naAleksanda Mkuu; lakininasaba zaWaparthia naWasasanidi waliendelea kufufua milki ya Uajemi tena na tena.

Baada yauvamizi wa Waarabu Ujaemi wkatawaliwa kwa muda kama sehemu yaukhalifa wa Uislamu lakini baada yakarne kadhaa nasaba za kieneo zilichukuautawala kwa jina lakhalifa ila hali halisi kama watawala wa kujitegemea.

Baada ya uvamizi waWamongolia nasaba ya wana waTimur iliunganisha Uajemi pamoja na Afghanistan na Asia ya Kati.

Tangu mwaka1600kitovu cha utawala kilirudi Uajemi wenyewe chini ya nasaba zaSafawi naKhadjari.

Baada yavita kuu ya kwanza ya duniaafisa wakijeshiReza Khan alimaliza utawala wa Wakhadjari akaanzisha nasaba yaPahlavi. Alijaribu kuleta matengenezo ya kimaendeleo nchini akaiga katika mengi mfano waAtatürk katikaUturuki jirani.

Utawala wa kifalme ulikwisha mwaka1979 wakati wa mapinduzi ya Kiislamu chini ya uongozi waAyatollahKhomeini yaliyoanzishaJamhuri ya Kiislamu.

Kipindi kifupi baada ya mapinduziUajemi ilishambuliwa na Iraki navita vya miaka 8 ilisababishavifo vingi.

Uhusiano nanchi za magharibi, na hasaMarekani, umekuwa mgumu tangumapinduzi, hasa baada ya wanafunzi Waajemi kushambuliaubalozi wa Marekani mjini Teheran na kuwateka Wamarekani kama makole.Fatwa ya Ayatollah Khomeini kudai kifo chamwandishiSalman Rushdie iliongeza sifa za ukali za Uajemi.

Tanguuchaguzi waRaisMahmoud Ahmadinejad mwaka2006 aliyetamka matishio dhidi ya nchi yaIsraeli kuna mashaka juu ya mipango ya Uajemi kupanuateknolojia yake ya kinyuklia kwahofu ya kwambaserikali yake inalenga kujengabomu ya nyuklia. Mapatano yalichukua miaka hadi kufikiwa mwaka2015.

Utawala

Uajemi ni Jamhuri ya Kiislamu inayoongozwa nakatiba yenye sehemu za kidemokrasia na sehemu za kidini.

Mamlaka kuu ikomikononi mwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi anayesimamiasiasa ya nchi kwa jumla; yeye niamiri jeshi mkuu na msimamizi mkuu wahuduma yausalama; pia anaratibu siasa ya nje. Anateua wakuu wa jeshi,redio natelevisheni, viongozi wasalat wamsikiti mkuu katika kilamji,jaji mkuu namwendesha mashataka mkuu halafu nusu ya wajumbe wa Halmashauri ya Walinzi wa Katiba wanaokubali au kukataa sharia zote zilizopitishwabungeni wakiwa na mamlaka kusimamisha wagombea kwa uchaguzi wa kitaifa. Anaweza kumwachisha rais. Kiongozi mkuu huchaguliwa na Mkutano wa Wataalamu wa Uongozi kwa muda wa maisha yake.Ayatollah Khamenei ni Kiongozi Mkuu wa pili tangu mapinduzi ya Kiislamu.

Serikali inayoongozwa na rais wa Uajemi aliye na nafasi ya pili baada ya Kiongozi Mkuu. Huchaguliwa na wananchi wote kwa kipindi cha miaka 4 na anaweza kuchaguliwa upya. Wagombea wanahitaji kukubaliwa na Halmashauri ya Walinzi wa Katiba. Rais anaongoza serikali na kazi yake. Katika mambo ya siasa ya nje, jeshi na siasa ya nyuklia yuko chini ya mamlaka ya kiongozi mkuu.

Bunge inayoitwa "majlis" inawabunge 290 waliochaguliwa kwa muda wa miaka 4. Wagombea wote wanahitaji kibali cha Halmashauri ya Walinzi wa Katiba. Majlis inatunga sheria za nchi na kukubalimakisio ya serikali na mikataba ya kimataifa. Sheria zote zilizopita bungeni zinahitaji tena kibali cha halmashauri ya walinzi.

Halmashauri ya Walinzi wa Katiba ni chombo muhimu sana kinachohakikisha mamlaka kuu ya kiongozi mkuu. Ina wajumbe 12 ambao niwanasheria. 6 wanateuliwa moja kwa moja na Kiongozi Mkuu. 6 wengine wanachaguliwa nabunge kati ya majina wanaopelekwa mbele na jaji mkuu - anayeteuliwa na Kiongozi Mkuu. Kwa hiyo kiongozi mkuu anaamua juu ya wajumbe wote waliomo katika halmashauri hii, hakuna anayeweza kuwa mjumbe bilakibali chake ama moja kwa moja au kupitia jaji mkuu aliyeteuliwa naye.

Mikoa

Uajemi umegawiwa kwamikoa 31 inayoitwa "ostan" chini yagavana anayeteuliwa na rais. Kila mkoa huwa nawilaya (shahrestan) na ngazi ya chini zaidi nimitaa (bakhsh). Chini ya mitaa kunakata (dehestan) zinazojumlisha vijiji kadhaa.

Watu

Iran ina mchanganyiko wa makabila na dini uliounganishwa nautamaduni nalugha yaKiajemi, ambayo inatumiwa na wananchi walio wengi na ndiyolugha rasmi, ikifuatwa na lugha nyingine za jamii yaKihindi-Kiulaya, lakini pia za jamii nyingine kamaKiazeri (16%) naKiarabu (2%) (angaliaorodha ya lugha za Uajemi).

Dini

Uajemi iliwahi kuwa nadini zake zaUzoroasta naUmani.

Kuanziakarne ya 4BK idadi yaWakristo ilikua.

Tangukarne ya 7WaarabuWaislamu walivamia Uajemi na kuifanya polepole kuwa nchi ya Kiislamu. Katikakarne ya 16Uislamu wa Kishia ulitangaziwa kuwadini rasmi nchini.

Leo hii takriban asilimia 90 za wakazi ni Waislamu Washia. Karibu 10% niWasunni, hasa katika maeneo karibu na mipaka; kiutamaduni Wasunni wengi niWakurdi,Wabaluchi auWaturkomani.

Wafuasi wa dini nyingine kwa jumla ni kama 1% ya wakazi wote. Kundi kubwa niBahai lakini dini yao ilipigwa marufuku baada ya mapinduzi ya Kiislamu. Kundi linalofuata ni Wakristoː kati hao kundi kubwa niWaarmenia, halafuWakaldayo.Wayahudi wa Uajemi ni kundi kubwa kati ya nchi zote za Kiislamu wamashariki ya kati (0.01%). Wazoroasta wamebaki pia (0.03%). Kundi dogo sana niWamandayo wanaoitwa pia wafuasi waYohane Mbatizaji.

Tazama pia

Tanbihi

  1. Statistical Centre, Government of Iran.""Population by Religion and Ostan, 1375 Census (1996 CE)"". Iliwekwa mnamo2006-04-14.
  2. "official population clock as of March 17, 2015".http://www.amar.org.ir/.

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo yaAsia

Afghanistan |Armenia2 |Azerbaijan |Bahrain |Bangladesh |Bhutan |Brunei |China |Falme za Kiarabu |Georgia2 |Hong Kong3 |Indonesia |Iraq |Israel |Jamhuri ya China (Taiwan) |Japani |Kamboja |Kazakhstan |Kirgizia |Korea Kaskazini |Korea Kusini |Kupro2 |Kuwait |Laos |Lebanoni |Macau3 |Malaysia |Maldivi |Mongolia |Myanmar |Nepal |Omani |Pakistan |Palestina |Qatar |Saudia |Singapuri |Sri Lanka |Syria |Tajikistan |Timor ya Mashariki |Turkmenistan |Uajemi |Ufilipino |Uhindi |Urusi1 |Uthai |Uturuki1 |Uzbekistan |Vietnam |Yemen |Yordani

1. Nchi ina maeneo katikaAsia naUlaya. 2. Nchi ikoAsia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi zaUlaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.


Makala hii kuhusu maeneo yaAsia bado nimbegu.
Je unajua kitu kuhusuUajemi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwakuihariri na kuongeza habari.
Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Uajemi&oldid=1226063"
Jamii:

[8]ページ先頭

©2009-2025 Movatter.jp